Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA AWAOMBA WANANCHI KUTOKUFANYA MAKOSA NOVEMBA 27 AWATAKA KUWACHAGUA WAGOMBEA WA CCM.



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amewaomba wananchi wa mkoa huo kuwachagua viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu ili waweze kushirikiana na viongozi waliopo kuwaletea maendeleo. 



Mbunge Zuena ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za serikali za mitaa ambapo kimkoa zimezinduliwa katika viwanja vya soko la Pasua kata ya Bomambuzi manispaa ya Moshi na Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa chama cha Mapinduzi, Rabia Hamid. 



Alisema kuwa, chama cha Mapinduzi kimefanya kazi kubwa ambapo viongozi wake wamepambana kuhakikisha mkoa huo unapata fedha nyingi za miradi ya maendeleo na kuwaomba wananchi kuwalipa kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na chama hicho. 



"Ndugu zangu wananchi tunayo sababu za kuwaomba muwachague viongozi wanaotokana na chama chetu kazi kubwa tumeifanya katika kipindi hiki na ninyi ni mashahidi sasa hatupaswi kufanya makosa katika uchaguzi huu tuwachague viongozi bora wanaotokana na CCM" Alisema Mbunge Zuena. 


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI