Header Ads Widget

MBUNGE NDINGO AMPA TANO DKT.TULIA KWA UWEZESHAJI KIUCHUMI WANANCHI

 



Na  Matukio Daima Media,App, Mbeya 


MBUNGE wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Mh, Bahati Ndingo amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson hakuna kundi ambalo ameliacha katika kuhakikisha kuwa  anawawezesha kiuchumi wananchi wa Jimbo hilo wakiwemo vijana,wanawake na wazee na kusema ni kiongozi wa mfano anayepaswa kuheshimiwa na kulindwa.


Ndingo amesema hayo November 14,2024 wakati Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini  na Rais umoja wa mabunge duniani (IPU)Dkt.Tulia alipokuwa akikabidhi nyumba za wahitaji watatu wanaoishi katika mazingira magumu kata za  Iyunga mtaa wa Inyala  na kata ya Ilemi Jijini Mbeya Mbeya.


"Hakuna kundi ambalo Dkt.Tulia  ameliacha katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo kuwezesha vijana pikipiki 100, na bado ni vijana wengi amewezesha kiuchumi,wazee bima za afya, wanawake wamewezeshwa mikopo ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji  kiukweli hata kwangu Mbarali ameweza kusaidia bila kujali kuwa sio Jimbo lake "amesema.


Hata hivyo Mbunge huyo amewataka viongozi wa dini kuendelea kumwombea Dkt . Tulia kuwa kama Dunia inamthamini na kumheshimu ni lazima wana Mbeya waone thamani yake na wamheshimu na kumsemea mema na kutangaza mambo mazuri anayofanya.


Akifafanua zaidi Ndingo amesema kuwa licha ya kuwa Dkt .Tulia  muda wake  umekuwa ni mdogo bado  kila anapopata nafasi lazima arudi Jimboni kwake kuangalia changamoto za wananchi wake na kuzitatua na zingine kunipeleka sehemu husika kwa utatuzi zaidi.


Aidha katika kumpa sapoti Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini ambaye alikuwa akikabidhi nyumba za wahitaji watatu wa kata za Iyunga na Ilemi wabunge wa  Jimbo la Mbarali  Bahati Ndingo na Mbunge wa Jimbo la Rungwe,Mwantona walikabidhi  shilingi 60,0000  za wahitaji hao ili waweze kupata muhimu.


Akielezea kuhusu mradi mkubwa wa maji wa  Kiwira Ndingo amesema mradi huo una  historia ya muda mrefu umetekelezeka kwasababu wana Rais umoja wa mabunge duniani,Spika wa bunge anayetoka Mbeya hivyo wana Mbeya msipuuze nafasi hiyo na kusema wana Mbarali na Rungwe, Chunya wanamwombea kila siku ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri.


"Sasa nyie hapa Mjini mkiendelea kukomaa kamanda na mtakomaa kweli sasa hivi tunataka maendeleo  Mbeya mjini sio kitu kingine maana kiongozi mmempata anagusa kila kundi hakuna kundi aliloliacha "amesema Mbunge Ndingo.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rungwe,Antony Mwantona amesema kwa umoja wao wataendelea kumuunga mkono Dkt.Tulia kwani licha ya kusaidiana makundi mbali mbali Jijini hapa bado amekuwa akisaidia hata wananchi wasiokuwa wa Jimbo la Mbeya mjini hivyo anapaswa kulindwa kwa nguvu zote.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI