Na, Matukio Daima App,
Wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga wanaofanya biashara katika katika soko la mlandege manispaa ya Iringa,
wamezua taharuki kubwa mara baada ya MACHINGA zaidi ya 600 kukimbia katika eneo Hilo na kurudi katika eneo la Mashine 3 ambako ndiko walipoondolewa mwanzo na serikali.
Wafanyabiashara wadogo maarufu, kama wamachinga mkoani Iringa, waliohamishiwa soko la mlandege watishia kurudi katika maeneo waliyotolewa awali, kwa madai ya kukosa wateja pamoja na viongozi wa mkoa kushindwa kusikiliza malalamiko yao.
Wamesema soko hilo jipya limepoteza mvuto kwa wateja kutokana na kukosa bidhaa za kutosha ukilinganisha na soko la mashine tatu ambalo wameondolewa awali, na hiyo inatokana na wateja wengi kushindwa kufikia eneo hilo.
Aidha, wamachinga hao wamesema wamekuwa kitoa malalamiko yao kwa uongozi wa mkoa Iringa, kwa muda mrefu bila mafanikio jambo ambalo limepelekea baadhi yao kuondoka katika soko hilo.
Mwenyekiti Machinga Smart Group Iringa,Yahaya Mpelembwa
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Machinga Smart Group, Yahaya mpelembwa, amesema jopo soko la Mlandege kuwa ni eneo zuri kwa wamachingao katika upande wa uasalama wao wa kiafya na ulinzi, lakini bado linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa wateja, kutokana na kuzungukwa na masoko mengi yanayofanya biashara kama hizo.
Mpelembwa, ameitaka serikali kuangalia upya soko hilo na namna ya kuliboresha kwa kufikisha vyombo vyote vya usafiri hasa vya mijini kwani hao ndiyo wanaonekana kuwa na uhitaji wa bidhaa za soko hilo zaidi.
Hata hivyo, ameishukuru serikali ya mkoa wa Iringa kwa kutumia migambo kupiga wafanyabiashara ambao wamerejea katika soko la mashine tatu.
Mstahiki Meya manispaa ya Iringa Ibrahimu NgwadaAkijibu Malalamiko hayo, Mstahiki Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahimu Gwada amekiri uwepo wa idadi ndogo wa wateja katika soko la Mlandege jambo ambalo limechangia wafanyabiashara hao kuendelea kukimbia eneo hilo pamoja na kuongeza kuwa, kwa sasa hawatatumia tena nguvu, kuwaondoa machinga katika ya mji kama ilivyokuwa awali.
Aidha, Mstahiki Meya Ngwada ametoa wito kwa wafanyabiashara hao wakuchukua tahadhari za kiusalama, kwani maeneo wanayotumia kufanya biashara hizo, si sahihi kwa usalama wao kutokana na kutumiwa na vyombo vya moto.






0 Comments