Header Ads Widget

KANUNI ZILIWAENGUA WAGOMBEA WALIOKOSA SIFA KIGOMA UJIJI - MABUBA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Kigoma mjini Kisena Mabuba amesema kuwa sheria na taratibu za uchaguzi ndizo zilizosababisha wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na wajumbe wa serikali za mitaa kukosa sifa na kuenguliwa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kigoma Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa mchujo huo kwa ajili ya kuchuja wagombea wenye sifa umevihusu vyama vyote 17 vilivyosimamisha wagombea kwenye uchaguzi huo ikiwemo CCM ambayo wajumbe wake pia wameenguliwa kwa kukosa sifa.

Bila kutaja idadi kwa vyama vyote alisema kuwa Chama Cha ACT Wazalendo ambacho kilisimamishwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na wajumbe kwa mitaa yote 68 ya jimbo la Kigoma Mjini wagombea wake tisa wameenguliwa kwa kukosa sifa.

Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa miongoni mwa vigezo vilivyowafanya wagombea hao kukosa sifa ni Pamoja na kushindwa kukamilisha maelekezo ya kujaza fomu za uteuzi na wengine kukosa sifa kwa sababu ya masuala ya utata wa uraia wao

 “Nafasi ipo wanaweza kuitumia siku ya Jumapili kukataa rufaa na kuleta mapingamizi yao kupinga kuenguliwa na ofisi ya msimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wake watakuwepo kupokea mapingamizi na kuyafanyia kazi kama ambavyo Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ametoa maelekezo,”Alisema Msimamizi huyo wa uchaguzi jimbo la Kigoma Mjini.


Akizungumzia kadhia ya kuenguliwa kwa wagombea wa chama chao Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kigoma Mjini wa Chama cha ACT Wazalendo, Frank Luhasha alisema kuwa walisimamisha wagombea Zaidi ya 400 kwa nafasi zote zilizotangazwa kwenye mitaa yote 68  ya jimbo la Kigoma Mjini lakini walioteuliwa ni wagombea 70 pekee.



Naye mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kigoma Mjini, Omari Gindi alisema kuwa katika chama chao nafasi ya Mwenyekiti wameenguliwa wagombea wanne na wajumbe  12 na kwamba sababu walizoambiwa za kukosa sifa kwa wajumbe hao siyo ya kikanuni yanayoweza kumuengua mgombea hivyo CHADEMA Taifa wametoa maelekezo kwamba watatoa tamko kuhusu jambo hilo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI