Header Ads Widget

CCM YAPONGEZA VIJANA KWA KUKIPAMBANIA CHAMA

 




VIJANA ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini wamepongezwa kwa kukipambania  na kufanikisha ushindi wa kishindo kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa.


Hayo yamesemwa kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella wakati akifungua mafunzo ya 13 ya uongozi vijana kutoka vyama sita vya Kusini mwa Afrika kuhusu masuala ya maendeleo.


Mongella amesema kuwa CCM ilitumia vijana kwenda kuwaambia vijana na wananchi namna ambavyo serikali ya awamu ya sita ilivyotekeleza ilani kwa lengo la kuleta maendeleo kwa nchi.


Naye mwakilishi wa CPC Wang Jiang amesema kuwa wanafurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya vyama hivyo ambapo China imeendelea kutoa fedha kwa nchi za Afrika kwa ajili ya masuala ya maendeleo.


Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Profesa Marcelina Chijoriga amesema kuwa mafunzo hayo ni kwa vyama sita ambavuo viko madarakani na vionaongoza ambavyo ni Anc Afrika Kusini, Ccm Tanzania, Frelimo Msumbiji, Mpla Angola, Namibia Swapo na Zimbabwe Zanu-Pf.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI