WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wametakiwa kupambana kuhakikisha wagombea wanaotokana na chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa wanashinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Novemba 27 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya halmashuri kuu ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Best Simba wakati alipokutana na makada wa chama hicho wilayani Rombo.
Simba alisema kuwa, jukumu la kila mwanaccm ni kuhakikisha wagombea wanaopeperusha bendera ya ccm katika uchaguzi wa serikali za mitaa wanashinda kwa kishindo hivyo amewataka kwenda kuwashawishi wananchi na kuwaomba wawachague viongozi wanaotokana na ccm.
Alisema kuwa, serikali imefanya kazi kubwa hivyo wanaccm wanawajibu wa kupita na kusemea kazi hizo kwa wananchi ili waweze kutambua kwanini wawachague viongozi wanaotokana na ccm.
"Uchaguzi huu ni kipimo chetu sisi wanaccm hivyo tushirikiane na tushikamane kwa pamoja kuhakikisha wagombea wetu wanashinda kwa kishindo Novemba 27 mwaka huu" Alisema Simba.
Mwisho..
0 Comments