Header Ads Widget

WAZIRI WA KILIMO NA RAIS SAMIA WASIKIE KILIO CHA WAKULIMA: HAONGA, ATAKA CCM IWAJIBIKE.

 


NA JOSEA SINKALA, SONGWE.

Mwenyekiti wa kamati ya Kilimo, mifugo na uvuvi wa bunge la wananchi Pascal Haonga, ameishukia Serikali kupitia wizara ya kilimo kushindwa kuwalipa wakulima na wafanyabiashara wa zao la mahindi fedha wanazodai ili kutowakwamisha kuzalisha mazao msimu ujao wa kilimo.


Haonga ambaye alikuwa mbunge wa jimbo la Mbozi mkoani Songwe (CHADEMA), amesema hayo kwenye mazungumzo yake juu ya kile anachoita Serikali kupitia wakala wa uhifadhi wa chakula cha Taifa (NFRA) kukopa mahindi kwa wakulima lakini mpaka sasa bado haijawalipa.


Amesema Serikali imekuwa ikinunua mahindi kwa wakulima na kwenda kuyauza nje ya nchi kwa faida badala ya kuweka mazingira rafiki ya biashara ambapo pamoja na mfumo huo bado imechelewa kuwalipa wale waliouza mahindi yao kwa muda wa miezi miwili iliyopita (kati ya Agosti - Oktoba).


"Ni jambo baya sana inalofanya Serikali, yaani inanunua mahindi kwa wakulima kwa kuwakopa kwa elfu sabini kwa gunia moja la kilo miamoja halafu Serikali yenyewe inaenda kuuza kwa shilingi laki moja inamaana inapata faida ya elfu thelathini badala ya kuweka mazingira mazuri wafanyabiashara wafaidike sasa inamaana wamegeuka kuwa madalali", amesema Haonga na kuongeza.


"Sasa kwa wakulima waliouza mahindi yao kwa miezi zaidi ya miwili iliyopita mpaka leo hawajalipwa fedha zao wakati Zambia walishailipa Tanzania inamaana madhara yake ni kwamba wakulima watashindwa kununua mbolea, mbegu na kuandaa mashamba", ameeleza Pascal Haonga, mbunge wa zamani wa jimbo la Mbozi.


Hata hivyo amesema Waziri wa kilimo Hussein Bashe anapaswa kujitafakari na kuwajibika ikiwemo kujiuzulu kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi wake ambao wameshindwa kupata stahiki zao huku wengine tangu mwaka jana (2023) wakiwa bado hawajalipwa fedha shilingi Billion mia tatu za usambazaji pembejeo za kilimo.


"Rai yangu kwa Waziri wa kilimo Hussein Bashe, naomba ujumbe huu umfikie, umfikie pia Rais Samia Suluhu Hassan na wahusika wote walipe hizi fedha haraka ili wakulima wajiandae na msimu ujao wa kilimo ingawa wamechelewa lakini wawalipe haki yao.


 Na pia msimu wa 2023/2024 (mwaka jana) kuna watu wa makampuni wale wanaosambaza pembejeo kama mbolea mpaka leo hii wanadai zaidi ya shilingi Billion mia tatu Serikali haijawalipa tafsiri yake taasisi za kifedha (benki) wakauze dhamana za wafanyabiashara hao maana wale wanafanya biashara. 


Sasa kwakuwa kuna mchakato unaendelea wa uandikishaji kwa muda mfupi uliosalia huu wakulima wa kanda ya nyanda za juu kusini na wa-Tanzania wote jiandikisheni ili Novemba 27, 2024 tukaanze nao kwenye Serikali za mitaa tukachague viongozi watakaotusaidia halafu mwakani tukawapige kwa madiwani, wabunge na Rais", amesema Pascal Haonga..



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI