Header Ads Widget

WAZIRI SIMBACHAWENE: HAKUNA KITU KIZURI KAMA MAISHA YA NDOAP

   

Na Hamida Ramadhan matukio Daima app DODOMA 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene (Mb) amesema maisha ya  ndoa ni mazuri huku akimtaka  Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mpwapwa 

Ndg.Mgutho Thabit Mathew aliyefunga pingu ya maisha na Mke wake  Herieth Kileo  kuishi maisha yenye  upendo na kujaliana. 


Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo wakati akizungumza  kama Baba Mzazi wa Ndg. Mghuto kwenye  sherehe hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpwapwa ambapo amewataka wakaishi maisha mema na kuijenga familia yenye heshima.



" Ndoa hii ni ushahidi tosha mbele za watu na mbele za Mwenyezi Mungu, naamini hamtatuangusha na hamfanyi utani tumieni  heshima hii ili watu hawa waliokuja hapa wasije kusema walipata hasara na  kupoteza muda wao bure" amesisitiza Waziri Simbachawene

Amewataka kujiepusha na tabia ya uongo ili waweze kujenga familia yenye ustawi na staha mbele ya jamii na Mwenyezi Mungu.

Katika hatua nyingine, Waziri Simbachawene ametoa wito kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza Mpwapwa katika sekta ya burudani kufuatia uhaba mkubwa  wa sehemu hizo hali inayopelekea wakazi wa Mpwapwa kukosa sehemu za kwenda kula maisha.


" Watu wa Mpwapwa wanakosa sehemu ya kwenda kula 'vibe' hivyo uwekezaji wa kipekee unahitajika  ili waweze kufurahia maisha " amesisitiza Simbachawene

Ndoa  hiyo ya Ndg. Mwenezi Mgutho Thabit Mathew na Ndgu Herieth Kileo ambayo  wamefanikiwa kufunga  Oktoba  27, 2024 katika Kanisa la Mtakatifu Paulo (St.Paul) wilayani Mpwapwa imehudhuriwa watu wengi  akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Dkt.Sophia Kizigo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI