Na,Jusline Marco;Arusha
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt.Godson Abel Mollel amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mazuri ili kuweza kuwalinda dhidi ya mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza kwenye maafali ya 9 ya wahitimu wa darasa la 7 katika Shule ya msingi ya mchepuo wa Kingereza ya Silver Meru iliyopo Wilayani Arumeru ambapo amesema elimu bora na ujuzi wa neno la Mungu utawawezesha kuchambua yaliyomema na kuyaacha yaliyomabaya.
Aidha amewataka kuwaendeleza watoto wao kimasomo kwani tayari hatua ya msingi imepita hivyo wawawezeshe kuyatimiza maono ambayo Mungu ameweka ndani yao, wakawe watu wa maana katika taifa na katika jamii inayowazunguka.
Vilevile ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa uwekaji wa ratiba ya ibada ya neno la Mungu hatua inayoonyesha kumtengeneza mtanzania mwenye kujifahamu,kujitambua ,mwenye kumuheshimu Mungu na mwanadamu.
Ameongeza kwa kuwataka wahitimu hao kuwa na ujuzi mwingine wa stadi za maisha ambao utamsaidia katika kuyaendesha maisha yake kwani ndiyo muelekeo wa sera ya taifa mashuleni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo amesema mpango na mkakati wa shule hiyo ni kuwafundisha watoto stadi za maisha ambayo itawawezesha wanafunzi kujifunza kazi za mikono na kuwa na ujuzi wa vitu mbalimbali,ambapo pia shule nyingi zina changamoto ya walimu kutokana na sekta hiyo kutowezeshwa na kupewa kipaumbele kama sekta nyingine.
Awali akizungumza katika maafali hayo Kamishna Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Polisi jamii katika Mkoa wa Arusha Peter Lusesa,amesema teknolojia au utandawazi umekuwa ukiwapotosha watoto wengi kwa sasa kutokana na wazazi kuwaachia mifa mwingi watoto simu za mkononi.
Naye Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Godwin Robert Mwalisiaka amesema shule hiyo tangu kuanzishwa imekuwa ikifanikiwa kukua kitaaluma kwa kutoa kiwango bora cha elimu kinachokidhi kuwaandaa wanafunzi kutatua changamoto mbalimbali katika jamii kwa kuzingatia viwango vinavyotolewa na wizara ya elimu nchini.
0 Comments