Header Ads Widget

WATUMISHI WA GACHAGUA KENYA KWENDA LIKIZO YA LAZIMA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA NAIROBI

MAMLAKA katika Ofisi ya Naibu Rais wa Kenya aliyeondolewa ma- darakani Rigathi Gachagua (pichani chini), imewaagiza maofisa 108 wa ngazi za juu katika ofisi hiyo. kwenda likizo ya lazima, wakiwa mo baadhi ya washauri wakuu wa Naibu Rais huyo.


Katika taarifa iliyotolewa jana, ilibainisha kuwa utekelezaji wa agizo hilo ulianza juzi, Jumamosi, saa 6:00 mchana, ikielezwa kuwa katika barua ya ndani ya usimam- izi, mamlaka hiyo pia imesitisha mikataba yote ya wafanyakazi wa kandarasi za muda.


"Maofisa wote walioorodheshwa katika vikundi vya kazi T na U wanaagizwa kwenda likizo ya lazima mara moja," ilisoma risala iliyoandikwa na Patrick Mwangi, Katibu Mkuu Tawala katika Ofisi ya Naibu Rais.

Risala hiyo ambayo pia nakala yake ilitumwa kwa mkuu wa utum- ishi wa umma wa ikulu, ilisema kuwa agizo hilo linatekelezeka kuanzia saa sita mchana, Juma- mosi.

Hii inakuja wakati Rais William Ruto, anakabiliwa na changamoto nyingine ya kumteua atakayeshi- kilia wadhifa wa Naibu Rais, huku kesi za kupinga chaguo lake ziki- wasilishwa mahakamani.

Wakati huo huo, Mahakama nchini humo iliagiza Ijumaa, kusit- ishwa utekelezwaji wa kumoundoa Gachagua kutoka ofisini pamo- ja na mchakato wa kumteua mrithi wake hadi Oktoba 24. mwaka huu, ambako kesi hiyo itaamuliwa mbele ya jopo la majaji watatu.

TRT

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI