Header Ads Widget

WAKILI WA MGOMBEA UPINZANI MSUMBIJI AUWAWA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA MAPUTO

EVINO Dias, aliyekuwa wakili wa mgombea mkuu wa up- inzani kwenye uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 9, mwaka huu, Venancio Mond- lane, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Maputo.

Wakili huyo, Evino Dias, ali- uawa kwa shambulio la risasi jana, pamoja na mgombea mwingine, Paulo Guambe wa chama cha PODEMOS, kina- chomuunga mkono Mond lane.

Mashahidi wa tukio hilo walisema watu wawili we- nye silaha walilifyatulia risasi gari la wawili hao, lililokuwa limeegeshwa kwenye bara bara katikati mwa mji huo mkuu.

Kiongozi wa chama cha PODEMOS, Albino Forquilha, alithibitishia vifo hivyo kwa shirika la habari la AFP, huku chama cha mawakili nchini humo kikieleza kushtushwa na mauaji ya Dias.

Polisi ilisema uchunguzi umeanzishwa lakini hai- kuthibitisha mara moja utambulisho wa watu hao wawili waliouawa.

Umoja wa Ulaya (EU), ume- toa taarifa ya kulaani mauaji

ya Dias na Guambe na kutoa wito wa uchunguzi kamili na wa wazi utakaowawajibisha wale waliohusika na uhalifu huo.

Ilielezwa kuwa hayo yana- jiri wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo ya uchaguzi am- bao umeshuhudiwa kuibua madai zaidi ya wizi wa kura na kubana upinzani, dhidi ya chama tawala kwa muda mrefu.


Aidha, wachambuzi wa masuala ya kisiasa walisema mauaji hayo ni ushahidi zaidi wa wazi wa ukosefu wa haki ambao wote wanakabiliwa nao.

PODEMOS ni chama kipya cha upinzani ambacho kilip- inga utawala wa miaka 49 wa chama cha 'Front for the Liberation of Mozambique(FRELIMO) katika uchaguzi wa Oktoba 9, mwaka huu.

Ingawa Mondlane aligom bea urais kama mtu huru, ali- ungwa mkono na PODEMOS Na kwamba wote waliungana na vyama vingine vya upin zani kuishutumu FRELIMO kwa udanganyifu katika uch- aguzi na kuvuruga uchaguzi.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa mgombea wa FRE LIMO, Daniel Chapo anashi kilia uongozi wa wazi katika kinyang'anyiro cha urais, ku tokana na matokeo ya awali.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yanatarajiwa ku tangazwa wiki ijayo na kwamba Chapo anatara- jiwa kutangazwa mshindi na kurithi mikoba ya Rais Filipe Nyusi, ambaye amehudumu.

@TRT

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI