Header Ads Widget

WASIOONA WAIUNGA MKONO ROYAL TOUR YA RAISI SAMIA KWA KUIPANDISHA FIMBO NYEUPE KILELENI

Na ESTHER MACHANGU, MOSHI

Katika kuadhimisha miaka 60 ya chama cha wasioona nchini Tanzania wamepanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuunga mkono Juhudi za Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha utalii wa ndani.

Habiba Ngulangwa ni mwenyekiti wa chama hicho amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwapa Fursa watu wenye ulemavu huo kutojiweka nyuma katika kushiriki shughuli za kijamii na pia kuiweka Fimbo nyeupe katika kilele cha Mlima huo mrefu barani Afrika ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya chama cha wasioona Nchini hapa.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa hatua hiyo itaongeza chachu kwa walemavu wa aina nyingine kupanda mlima huo ili kuionyesha jamii kuwa wanauwezo wa kushiriki katika matukio mbalimbali ya Kitaifa.

Hata hivyo mmliki wa Kampuni ya Kitalii ya Kilibase Adventure Mr Sifael ameambatana na wasioona hao wawili pamoja na muangalizi wao mmoja ambao jukumu lao ni kuhakikisha fimbo hiyo nyeupe inafika kileleni salama.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya ni Upatikanaji wa Teknolojia saidizi na Sikivu ni Mkombozi kwa Mtanzania Asiyeona.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI