Header Ads Widget

TASAF YAWEZESHA WANANCHI KUJIKWAMUA KIUCHUMI,WANUFAIKA WATOA USHUHUDA

 

Na Friday Simbaya, Mbeya

Msafiri Luaga, mkazi wa Kata ya Iziwa, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, amesema ruzuku za TASAF zimemsaidia kujenga nyumba ya kisasa baada ya kuondokana na makazi ya nyasi. Luaga pia alieleza jinsi fedha hizo zilivyomuwezesha kuwapatia watoto wake mahitaji muhimu ya shule na kununua mbolea za kilimo, hatua iliyompatia mavuno bora na kipato cha ziada. Pia alinunua ndama ambaye anafuga hadi sasa.

"Maisha yangu yamebadilika sana kupitia TASAF, watoto wangu sasa wanapata mahitaji ya shule, na pia nimefanikiwa kujenga nyumba ya kisasa," alisema Luaga.

Ofisa Habari wa TASAF, Meleckzedeck Nduye, alieleza kuwa mfuko huo siyo tu unatoa ruzuku bali pia hutoa elimu ya kujiwekea akiba kupitia vikundi vya wanufaika. Katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha, wanufaika wa TASAF walionesha bidhaa walizozalisha, ikiwa ni pamoja na sabuni za mwani kutoka Unguja na mikeka iliyo fumwa kitaalamu

Bishara Nassoro, kutoka Zanzibar, alieleza jinsi alivyonufaika na TASAF kwa kuanzisha biashara ya usindikaji wa bidhaa za baharini. "Ruzuku za TASAF zimenipa mtaji wa kuanzisha shughuli za ujasiriamali, na maisha yangu yamebadilika sana," alisema Bishara, huku akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuinua uchumi wa wananchi kupitia serikali ya awamu ya sita.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI