Header Ads Widget

CCM MANYONI YAMPA HEKO RAIS DK.SAMIA KWA KUMIMINA MABILIONI FEDHA ZA MIRADI

 


Na Thobias Mwanakatwe, Manyoni

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida, kimempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mabilioni  ya fedha yaliyopelekwa katika wilaya hiyo kwa ajili ya kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inawanufaisha maelfu ya wananchi.


 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Makhanda, ametoa pongezi hizo jana mbele ya Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Mlowa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

 “Tunamshukru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa miradi yote ambayo ametuletea, Wilaya ya Manyoni ina asilimia 55 ya ukubwa wa Mkoa wa Singida lakini hakuna kata ambayo haina mradi,” alisema Makhanda.

 Makhanda alisema katika kata 32 na vijiji 97 za Wilaya ya Manyoni  hakuna mahali ambako fedha hazijapelekwa na hii inaonyeshani jinsi gani serikali ya CCM inavyowajali wananchi wake kwa kuwaletea miradi ya maendeleo.

 Mwenyekiti huyo alisema kwa kuwa imani ya watu wa Wilaya ya Manyoni ni kulipa wema hivyo wataulipa wema huo kwa kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kura za kutosha.

 Alisema wataanza kutekeleza wema hup kwa kuanzia katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 na Uchaguzi Mkuu  utakaofanyika mwakani 2025.


 Naye Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Silaa, alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan mambo makubwa ya maendeleo yamefanyika nchini nzima .

 Silaa aliwaomba wananchi wenye sifa kujitokeza kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na wajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi ili kutimiza demokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI