Header Ads Widget

WANAWAKE VIJANA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KATIKA UFUGAJI WA KUKU KISASA



Na Esther Machangu, Moshi.


Ushirikishwaji wa vijana katika Sekta ya mifugo nchini imetajwa kuwa ni chachu katika ustawi wa mendeleo ya mwanamke kijana.


Hayo yamebanishwa katika Seminar hizo zinaendeshwa na Shujaaz kwa ushirikiano na Shirika la kimataifa la utafiti wa mifugo (ILRI) mkoani Kilimanjaro na Kagera na lengo kubwa ni kubaini vikwazo vya kijamii na kijinsia vinavyowakabili wanawake katika biashara ya ufugaji wa kuku na namna ya kuvitatua kwa kushirikiana na jamii zao.


Lucky komba kutoka katika jukwaa la SHUJAAZ amebanisha kuwa jamii kwa ujumla inayo nafasi ya kutengeneza mazingira wezeshi kwa wanawake vijana kushiriki katika shughuli za mifugo hasa ufugaji wa kuku, kwa mapana zaidi. 


Semina hizi zinazoendelea katika wilaya ya Hai na Siha, zimeibua vikwazo kadhaa ambavyo vinawakumba wanawake wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, vikiwemo vikwazo vya kijinsia ambavyo vinawazuia wanawake wengi kuwa na maamuzi yao wenyewe katika kufanya biashara hii. Vikwazo hivi vinazuia maendeleo yao kwenye kiuchumi na hata kuzuia wasichana wadogo ambao bado hawajaingia kwenye ufugaji, kuamua kuingia kwenye ufugaji.


Kwa upande wake Fraten Mtika ambayo ni Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro amesema kwa sasa tayari kuna kikundi cha wanawake ambao wamejikita katika kuzalisha vifaranga kutoka siku moja mpaka mwezi mmoja ndipo huvipeleka sokoni na hii humrahisishia mfugaji kuvitunza vyema na kupata matokeo mazuri kwani wafugaji wengi bado hawajaweza kufuga kifaranga cha siku moja. 


Pia ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana na jamii nzima kutatua changamoto zote za kijamii, kuanzia elimu mpaka changamoto za kijinsia ili wanawake wafanye vizuri kwenye ufugaji wa kuku.


Baadhi ya vijana walioshikiri katika semina hiyo Aisha Ramadhani na Rahma Mussa wamekiri kupatiwa mbinu mmbadala za kufanya kilimo na ufugaji ambapo hapo awali walichukulia shughuli hizo kuwa ni za wazee tu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI