Header Ads Widget

WANANCHI MKOANI LINDI WAMESISITIZWA KUENDELEA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MKAZI ILI WAWEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Khajaty Zainabu Telack amewaongoza wananchi kufanya mazoezi katika bonanza lililofanyoka leo huku lengo kuu likiwa kuhamasiaha kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Telack amewaomba wananchi ambao bado hawajajiandikisha waende wakajiandikishe ili waweze kushiriki zoezi la kupiga kura siku ya tarehe 27/11/2024.

"Tunamshukuru Mungu tumefika salama wote hakuna aliye dondoka.Niwasihi tuendelee kufanya mazoezi kwa afya zetu.


Uandikishaji unaendelea niwaombe wote ambao hamjajiandikisha muende mkajiandikishe hata mnao toka Mtwara"amesema Telack

Telack amewaomba wananchi wa Lindi pamoja na Mtwara waliojitokeza kushiriki Bonanza waende kujiandikisha na wenye sifa ya kuchaguliwa muda utakapofika wajitokeze kuchukuwa fomu ili wagombee.


"Muende kwenye maeneo yenu mkajiansikishe ili mpate viongozi watakaoenda kuungana na Rais kuleta maenseleo katika nchi yenu.Niwaombe wenye sifa ya kuchaguliwa muende mkachukue fomu ili muende mkaombe kuchaguliwa wakati utakapofika"amesema Telack mkuu wa mkoa wa Lindi.

Pia Telack amewasisitiza Wote watakao  jiandikisha siku ikifika waende wakapige kura na Wanafunzi waliofikisha sifa za kupiga kura waende wakajiandikishe.


Kwaupande wake mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria  Mwanziva amewapongeza washiriki wote kwa kujitokeza kushiriki Bonanza hilo lililounganisha watu kutoka makundi mbalimbali na ameahidi kuendelea kuwaunga mkono Lindi Jogging Club ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa bonanza hilo.

"Mazoezi ni afya mazeizi ni tiba nimewaelewa nitazidi kuwaunga mkono naomba niwe mjumbe na mwanachama. Mkazidi kuhamasishana watu wafanye mazoezi" amesema Mwanziva mkuu wa Wilaya ya Lindi.


Akisoma risala iliyo andaliwa na Lindi Jogging Club Hassani Makwela mmoja wa wanachama wa club hiyo amemuomba mkuu wa Mkoa awasaidia kupata ofisi pia wamemuomba awe mlezi wao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI