Header Ads Widget

WANANCHI 250,000 WANATARAJIWA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MULEBA

 


 Mariam Kagenda_Kagera


Jumla ya wananchi 250,000 katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wanatarajia  kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaaa  na vijiji utakaofanyika  Novemba 27 mwaka huu.



Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Muleba Isaya Mbenje ametembelea   vituo mbalimbali vya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura ulioanza leo na  kuzunguma na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa  Wilaya ya Muleba Ina kata 43 na vijiji 166 huku vituo vilivyotengwa kwa ajili ya zoezi la uandikishaji vikiwa  ni 802.



Amesema kuwa mpaka sasa maandalizi  yamekamilika  na vituo vyote vimefunguliwa huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi  watakaowaletea  maendeleo.




Mkuu wa wilaya ya Muleba  Dr Abel Nyamahanga  amesema kuwa anatambua  Wilaya ya Muleba  imezungukwa na visiwa vingi hivyo ametoa wito kwa ambao sio wakazi wasishiriki  zoezi Hilo kwani zoezi Hilo linawahusu wakazi wenyewe wa eneo Hilo kwenye Vitongoji na vijiji husika.


"Tunawingi wa visiwan na maeneo yetu kunawafanyabishara wengi wanakuja katika visiwa vyetu , tunahamasisha shughuli ziendelee lakini kama sio mtanzania au mkazi  usidhubutu kujiandikisha katika Daftari au  kushiriki uchaguzi huo.



Jilala chobo mwananchi wa kitongoji Bugombe  Wilaya ya Muleba amesema ili wananchi wawapate viongozi wanaotaka  wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha  kwani maamuzi pekee ya kumpata kiongozi wa kweli  ni kujiandikisha ili usubiri kupiga kura Yako.


"Wanachi wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kiongozi afai lakini hawajui kuwa namna pekee ya kumpata kiongozi Bora ni kujiandikisha na kujitokeza kumpigia kura  hivyo nawashauri wananchi wenzangu wajitokeze kujiandikisha "alisema Chobo.



Wakala wa Chama Cha Siasa Hassan Ayub akiwa katika kituo Cha uandikishaji cha Kijiji Magata  alipongeza utaratibu  uliowekwa na serikali katika maswala ya uandikishaji kwa kuhakikisha Kila mwenye haki ya kujiandikisha anapata Fursa ya kujiandikisha  bila kubuguziwa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI