Header Ads Widget

MKUU WA MKOA TANGA AZINDUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA.



NA AMINA SAIDI,TANGA.


MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani amezindua na kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura linaloanza leo October  11 ,2024 ambapo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vilivyoandaliwa ili kupata haki yao ya kikatiba.


Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Raskazone  kata ya Central jijini Tanga Balozi Buriani amewahimiza Wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vyilivyoandaliwa  wakiwa na vitambulisho vya Taifa, Bima ya Afya , Leseni za Udereva au passport za kusafiria.



Balozi Buriani ameongeza kuwa Serikali Mkoani Tanga imejipanga kuhakikisha zoezi Hilo linafanyika kwa wakati huku akiwataka Makarani kutokuwa kikwazo.


Aidha amesema kuwa zoezi hilo ambalo litadumu kwa muda wa siku 10  litafwatiwa na siku saba za uhakiki wa taarifa za mwananchi  katika daftari la kudumi la mpiga kura kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November  27,2024.


Amebainisha kuwa jumla ya Wananchi Milion 1.4  wanatarajiwa kuandikishwa katika vituo zaidi ya 5000 kata 245 vijiji 763 na vitongoji 4528,


"Tunamatumaini kuwa Wakazi wa maeneo husika wataendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika vituo vilivyoandaliwa katika maeneo yao,tukumbuke kuwa hii ni haki ya kikatiba kwa mtu yeyote mwenye sifa zakuchagua na kuchaguliwa kujitokeza kushiriki Uchaguzi huu wa Serikali za mitaa" Aliongeza Batilda 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI