Matukio daima media yashinda tuzo ya uandishi bora wa habari za maadhimisho ya hifadhi ya taifa ya ruaha iliyopo mkoani Iringa.
Tuzo hiyo ambayo imetolewa leo, na Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha, Kamishna msaidizi mwandamizi, Godwell Ole Meing'ataki yenye lengo la kutambua mchango wa waandishi wa habari mkoani Iringa katika uandishi wa habari za maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi hiyo, ambayo kilele chake kimehitimishwa october 7 mwaka huu.
Mwandishi wa habari wa Matukio Daima media, Francis Godwin ndiye ameibuka mshindi kwa kushika nafasi ya kwanza katika tuzo hizo, kwa kuchapisha makala na habari 40 zilizohusu maadhimisho hayo.
Makala na habari hizo ambazo zilichapishwa kupitia matukio daima media, pamoja na vyombo vingine ambavyo vinafanya kazi kwa kushirikiana na matukio daima media.
Akikabidhi tuzo hizo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha, Godwell Ole Meing'ataki, amesema, maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi ya taifa ya ruaha yalitambulika na kuzungumziwa na watu mbali mbali kutokana na juhudi za waandishi wa habari.
"Nilipigiwa simu na watu mbali mbali wakiniuliza hivi kuna nini huko Ruaha, hii yote ni kutokana na ufanyaji wenu wa kazi kwa moyo bila ya kutarajia malipo yoyote"alisema Ole Meing'ataki.
"Japo najua si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari mkoa wa Iringa kupongezwa kwani hata huko nyuma tulishawahi kushirikiana namna hii na kufanya kazi nyingi tu na kupelekea kupewa tuzo kutokana na bidii na moyo wa kujitoa.
Kwa upande wake, Francis Godwin, ameshukuru uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kuona mchango wa wanahabari katika kufanikisha maadhisho hayo, huku akiwa kumbusha waandishi kudumisha ushirikiano kati Yao ili kufikia malengo yao.
Waandishi wengine ambao wameshinda tuzo hizo ni mwaandishi wa habari wa redio shamba, Christina Ndokele, ambaye ameshika nafasi ya pili, nafasi ya tatu Edwin Dugange toka redio Ibony, nafasi ya nne Mohammed Nyaulingo wa Azam media na nafasi ya tano ikishikwa na Leila Kazimoto toka redia Furaha.
0 Comments