Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI IRINGA WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA HIFADHI YA RUAHA KUTOA ELIMU KULINDA MTO RUAHA MKUU



NA DUGANGE EDWIN

Viongozi wa Dini Mkoa wa Iringa Wameahidi Kushirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Kutoa Elimu ya Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji na Ulinzi wa Mazingira Ili Kulinda Mto Ruaha Mkuu Unaotegemewa Katika Ikolojia ya Hifadhi Hiyo.

Ahadi Hiyo Imetolewa Hii Leo Wakati wa Ziara ya Viongozi Mbalimbali wa Dini Mkoa wa Iringa Ndani ya Hifadhi Hiyo Ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Tangu Kuanzishwa kwa Hifadhi Hiyo ya Pili kwa Ukubwa Nchini.

Viongozi Hayo wa Dini Wametoa Ahadi Zao Mara Baada ya Kushuhudia Athari za Shughuli za Kibinadamu, Uharibifu wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi Yaliyosababisha Kupungua kwa Kiwango cha Maji Tiririka Katika Mto Huo.

Sheikh wa Wilaya ya Iringa, Salum Mwahuta, Amesema Wameshuhudia Kupungua kwa Maji Tiririka Katika Mto Ruaha Mkuu na Jinsi Wanyama Wanaoishi Majini na Viumbe Wote Hai Wanavyotaabika Ndani ya Hifadhi.

Sheikh Mwahuta Amesema Wataendelea Kutoa Elimu kwa Waumini Wote wa Kiislamu Kuhusu Umuhimu wa Kulinda Vyanzo vya Maji Vinavyoulisha Mto Ruaha Mkuu Ambao ni Chanjo Kikuu cha Maji Katika Hifadhi ya Ruaha.

Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekosti Mkoa wa Iringa, Askofu Ezekiel Mwenda Ameonesha Kusikitishwa na Wananchi Wanaochepusha Maji Katika Vyanzo vya Mto Huo na Kupelekea Kukauka Msimu wa Kiangazi.


Makamu Askofu wa Kanisa la Orthodox Mkoa wa Iringa, Father Dimitrios Nziku Amesema Viongozi Hao wa Dini kwa Umoja Wao Watatumia Nafasi Zao Katika Jamii Kuhamasisha Waumini Juu ya Umuhimu wa Kuhifadhi Mazingira.

Afisa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi Hiyo, Muikolojia Rehema Kaitila, Akizungumza na Viongozi wa Dini Amesema Tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Limeanza Kuchukua Hatua Kunusuru Kukauka kwa Mto Huo.

Kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu Kumekuwa na Athari Kubwa Katika Hifadhi Hiyo na Kupelekea Wanyama Kutembea Umbali Mrefu Kutafuta Maji na Hata Kutoka Nje ya Hifadhi na Serikali Kulazimika Kuchimba Mabwawa ya Muda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI