Header Ads Widget

NI WAKATI WA VIJANA NA SHUJAAZ


Na Esther Machangu, Moshi

Vijana zaidi ya 40 wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamepatiwa mafunzo ya ufugaji wa kisasa na Kilimo bora ambayo yatachochea vijana hao kuanza kufanya shughuli hizo kwa wigo mpana.

Vijana hao ambao wamekutanishwa na Shirika la Shujaaz leo October 24.2024 wilayani hapa wamesema elimu ya ufagi wa kisasa na kilimo imekuwa nyuma hasa kwa upande wao na hii ni kutokana na vijana wengi kuchukulia kama kilimo na ufugani ni kazi za wazee.



Abbas Abdi na Aisha Mmbaga ni moja ya vijana walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema ili Taifa liweze kuendelea ni vyema vijana wakashiriki katika shughuli za maendeleo hasa za kilimo na ufugaji wa kisasa.
Hata hivyo wameongeza kuwa ni muhimu kukawa na ushirikiano kati ya vijana wa kike na wakiume katika kuyafikia malengo ya pamoja ya kuinua uchumi wa vijana wote.

Kwa upande wake Afisa Mifugo na uvuvi wilaya ya Hai Fratern Mtika amesema kuwa tayari katika wilaya hiyo wameshapata kikundi kimoja cha wanawake wanozalisha vifaranga na kukitunza kutoka umri wa siku 1 mpaka mwezi 1 na Kisha kukuiza kwa mteja.


Hata hivyo ameongeza kuwa Wilaya ya Hai imejipanga kuanza kuongeza mnyororo wa dhamani wa bidhaa hiyo ya kuku kwa kufungua mabucha ya kitoweo hicho na  kuuza kwa Kilogramu.

Lucky Komba ni Afisa Mradi wa Binti SHUJAAZ Kutoka Jukwaa  la SHUJAAZ ambapo linajihusisha na kutoa elimu, ufahamu, na maarifa kwa vijana ili kuwasaidia kujitegemea na kufanikiwa katika maisha yao.

Lucky amesema ni vyema jamii ikatambua changamoto wanazokutana nazo wanawake vijana katika sekta ya ufugaji na Jinsi ya kuzitatua ili kuongeza ushiriki wa wanawake vijana.



SHUJAAZ hutoa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na vipindi vya redio, matangazo ya SMS, na tovuti ili kufikia vijana kote nchini Tanzania. Lengo kuu la SHUJAAZ ni kuelimisha na kuwahamasisha vijana kutumia vipaji vyao, kufanya kazi kwa bidii, na kujenga uwezo wao ili waweze kufikia mafanikio katika maisha yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI