Na Matukio Daima App,Mbeya
MAMLAKA ya usimamizi wa bima Tanzania Nyanda za juu kusini(TIRA) imesema kuwa imejipanga kikamilifu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kukuza soko la bima na kudumisha ufanisi na ulinzi kwa wakata bima waliopo katika maeneo mbalimbslo hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa October 23,2024 na Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania Nyanda za juu kusini ,Neema Lutula wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya huduma za fedha kitaifa inayofanyika Jijini Mbeya katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.
"Bima ni mkataba kati ya mkata bima na mtoa bima ili kuweza kuhakikisha athari za vihatarishi kutoka kwa mkata bima ili zisiweze kutokea ndo sababu tupo kwenye maadhimisho na tumejipanga kutoa elimu kwa umma na kuwahasa wananchi kutembelea Banda letu kupata elimu .
Hata hivyo Meneja Lutula amesema kwamba bima hizo huwa msaada mkubwa katika kuhakikisha mkataba bima anapata kinga ya athari ya majanga mbalimbali ambayo yanaweza kumpata yeye binafsi au shughuli zake za kiuchumi .
Mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda la Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA)Angelina Lukosi amesema ameweza kujifunza vitu vingi baada ya kupata elimu katika banda hilo ambavyo vimemfungua na kujifunza.
0 Comments