Na Matukio Daima media
Shirika la umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi ma Utamaduni(UNESCO) limeviomba vyombo vya habari nchini kutoa fursa sawa kwa kujumuisha watu wenye ulemavu na wanawake katika kutoa habari .
Mkuu wa Mawasiliano na habari wa UNESC0 -Tanzania,Nancy Angulo alitoa wito huo jana alipotembelea ofisi za taasisi ya wanahabari ya MAIPAC jijini Arusha.
MAIPAC ni Taasisi dada na Serengeti Media yenye makao makuu wilayani.Serengeti ambazo taasisi.zote zimekuwa na miradi kadhaa ya kijamii.
Angulo alisema vyombo vya habari vinapaswa wakato wote kutoa fursa kwa makundi yote katika jamii kupaza sauti katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
"Tunaomba katika kazi zenu msiwabaguwe ama kuwatenga watu wenye ulemavu na wanawake kwani mara nyingi sauti zao zimekuwa.hazisikiki amefurahishwa na jinsi MAIPAC inavyotumia vyombo vya habari kutekeleza miradi yake.
Hata hivyo, Angulo alipongeza MAIPAC kwa kufanyakazi nzuri kusaidia jamii za pembezoni kupitia vyombo vya habari.
Alisema MAIPAC ndio taasisi pekee ya waandishi wa habari nchini ambayo inafanyakazi na jamii za pembezoni moja kwa moja .
"Nawapongeza MAIPAC mnafanya kazi nzuri na muendelee kufanyakazi na radio za kijamii na wanahabari kusaidia jamii"alisema
Alisema MAIPAC pia inapaswa k kusaidia kuelimisha kupinga matukio ya ukatili dhidi ya walemavu,wanawake na watoto katika jamii.
"Kuelekea uchaguzi mkuu ni vyema katika kazi zenu kuzingatia maoni ya makundi yote ya jamii wakiwepo watu wenye ulemavu na wanawake"alisema
Angulo pia alipongeza mpango kazi wa MAIPAC juu ya kuongeza ushiriki na Utetezi wa watu wenye ulemavu,wanawake na watoto katika masula kadhaa na kijamii.
Awali ,Mkurugenzi mtendaji wa MAIPAC Mussa Juma na Meneja utawala wa MAIPAC ,Andrea Ngobole waliomba UNESCO kushirikiana na MAIPAC katika miradi yake kadhaa hapa nchini.
Juma alishukuru UNESCO kwa kuwaalika watendaji wa MAIPAC katika mafunzo juu ya masuala ya jinsia na utetezi na ushiriki wa watu wenye ulemavu,wanawake na watoto ambayo yalishirikisha radio za kijamii za kijamii na Idara ya habari (MAELEZO)
"Tumejifunza mengi na tunaimani kutumia elimu vizuri ikiwepo kuandaa vipindi maalum ,makala na machapisho kuhamaisha ushiriki sawa wa watu wenye ulemavu,wanawake katika jamii pia kupinga ukatili dhidi ya watoto"aliu
Ngobole alisema MAIPAC itaendeleaq kufanyakazi kwa weledi katika kufanya utetezi na uchechemuzi wa mambo ya kusaidia jamii.
Mwisho
0 Comments