Header Ads Widget

MAKALA :UKATILI WA MITANDAO UBAVYOWATAFUNA VIONGOZI WANAWAKE WA VYAMA VYA SIASA

Na Nihifadh Abdullah,Matukio Daima media Zanzibar 

Adhma yakufikia usawa wakijinsia kwa karne ya 21 imekuwa ni agenda inayotiliwa mkazo kimataifa na kitaifa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kiuchumi na kisiasa.

Jitihada mbalimbali  zinachukuliwa siku hadi siku za kuona kunapatikana  usawa wa kijinsi wa 50/50 nafasi za uongozi hii ikijumuisha na idadi iliyopo  ya wanawake 974,281 ambayo ni  sawa na asilimia  51 ikilingalishwana wanaume ambao ni 915,492 sawa na asilimia 49 kwa mujibu wa  sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 kwa  Zanzibar.

Jamii,familia na vyama vya siasa vikiwa na changamoto ila suala jengine ni mitandao ya kijamii ambalo linawarudisha nyuma zaidi wanawake kusonga mbele kwa kile kinachoonekana ni ukatili wa kimtandao.



Sharifa Suleiman ni Kaimu Mwenyekiti Taifa wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA) ambae pia alikua mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Amani mwaka 2020,amekiri uwepo wa ukatili unaowapata viongozi wanawake .Akiwa mhanga wa haya Sharifa anasema “Hii hali ishawapata viongozi wengi wanawake wa kisiasa na kiukweli haifurahishi kama mimi mara nyingi nikiitisha mkutano wa waandishi wa habari au kuweka kitu mtandaoni hutokea baadhi ya watu kuzodoa lakini naona ni hali kawaida kwa vile chama changu kinatupa mafunzo mbalimbali  ya uongozi yamenijenga kuwa madhubuti kuhusu matumizi ya mtandao” Amesema Sharifa.

Sharifa anaendelea kusema kuwa maoni mengi anayoyapata kwenye mitandao ni kuhusu nafasi yake ya kuwa kiongozi” Yaani naonekana kama sifai au kuweka kitu mtandaoni si haki yangu kuwa kwenye mtandao” Amemaliza Sharifa.

Hadi mwaka 2023, takriban watu milioni 10.5 nchini Tanzania wanatumia mitandao ya kijamii. Majukwaa maarufu kama na Facebook, WhatsApp, Instagram, na TikTok, ambayo yanatumika zaidi kwa mawasialiano, burudani, na biashara,huku wanawake takriban 40-45% ambapo ni zaidi ya milioni 5 ya wanawake wanaotumia intaneti nchini Tanzania

Kwa mujibu wa ripoti ya Maalumu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 iliyotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar – TAMWA ZNZ inaeleza kuwa, nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar wanawake ni asilimia 16 ambao ni nane tu, huku huku wabunge wanaowakilishaZanzibar wanawake ni wanne sawa na asilimia 8, Mawaziri wakiwa ni sita sawa na asilimia 33 na Makatibu wakuu ni saba sawa na asilimia 39.

Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa mwanamke ni mmoja tu sawa na asilimia 20, Wakuu wa Wilaya ni wanne sawa na asilimia 36 na Masheha wanawake ni 68 sawa na asilimia 17 kwa masheha wote ambao ni 389.

Tunu Juma Kondo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake -UWT wa Chama Mapinduzi CCM amesema janga la ukatili wa mtandao ni changamoto ambayo baadhi ya viongozi wanawake wa CCM wamekumbana nayo“Hii inanyongonyesha sana na wanawake wengine hurudi nyuma kwa woga kwani husemwi sana na kupewa sifa mbata ile huathiri sana nguvu ya uthubutu kwa wanawake”Amesema Tunu.



Ukatili wa  mtandao dhidi ya viongozi wanawake wa vyama vya siasa ni tatizo linaloathiri  siasa na jamii kiujumla  kwani mara nyingi hulenga kuharibu sifa ya viongozi hao na hata kashfa ambazo hazina ukweli.

Dkt Mzuri Issa ni Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA -ZNZ amesema ukatili wa mitandao unaowalenga wanawake ni miongoni mwa udhalilishaji kwani hali hio imekuwa ikiwazuia baadhi ya wanawake kushiriki kikamilifu katika siasa kwa kuhofia unyanyasaji.“Watu washindane kwa hoja nasio kudhalilishana hususan kwenye majukwaa ya kimitandao hali hii inawaumiza sana wanawake”Amesema Dkt Mzuri huku akiwataka wanawake waliopo kwenye siasa wasivunjike moyo na wasiogope kupigwa mtandaoni.

Sheria ya uchaguzi ya Rais wa Jamhuri Bunge na madiwani inazungumza kuwa ukatili wa wanawake ni uhalifu hivyo wakati umefika  kuchukuliwa hatua muafaka kwa wale wanaodhalilisha kwa  kuwavunjia heshima na utu  sambamba na vyombo husika kusimamia sheria za makosa ya mitandao hii itaondoa hofu kwa wanawake na wanafanya ukatili huo kubadilika. 

Afisa Msajili wa vyama vya Siasa Zanzibar Abdul-Razak Said Ali amesema uwepo wa sheria inayosimamia makosa ya mitandao Tanzania, ya mwaka 2015 lengo ni kuhakikisha ulinzi wa wanawake na unyanyasaji mitandaoni

 “Masuala yote kuhusiana na makosa ya kimtandao yanadhibitiwa juu ya sheria hiyo lengo ni kuwasadia wanawake wanapata haki zao pindi wakikumbana na ukatili kwenye mitandao” Amesema 

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Tech  and Media Converagency kupitia mpango wao wa Wanawake wanaotumia Teknolojia kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake mwaka 2022 ulibaini  kuwa asilimia 79 ya wanasiasa wanawake wanaotumia mitandao ya kijamii nchini Tanzania walifanyiwa ukatili wa aina mbalimbali kupitia mitandao 

Aidha utafiti  huo uliojumuisha vitendo vya kuvunjwa kwa faragha, lugha ya matusi pamoja na vitisho ulibaini pia zaidi ya asilimia 70 ya viongozi wanawake waliacha kutumia mitandao ya kijamii  kutokana na unyanyasaji wa mitandaoni hali ambayo imesababisha kudhoofisha jitihada zao za kushiriki kikamilifu katika siasa. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania - TCRA Dkt. Jabiri Bakari amesema mamlaka hio inaendeleza kutoa elimu ya masuala ya kidijiti na usalama mtandaoni kwa kuhakikisha  mazingira salama na imara ya matumizi bora ya mitandao.

”Ingawaje mipango ya kuongeza uelewa wa umma ni ajenda ya kudumu ya TCRA, kampeni hii inatokana na umuhimu wa kipekee kuwapatia Watanzania mbinu za kujilinda dhidi  ya mashambulio ya mitandao ya intaneti na simu  niwaombe hii pia  ni kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni”

 Amesema hayo Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi wa kampeni  ya “Ni Rahisi Sana” inayolenga kuelimisha Wananchi na  kwamba mazingiza salama mtandaoni.

Mwanaharakati kutoka vuguvugu la ukombozi wa Mwanamke Duniani   kwa Tanzania Rahima Mussa Hassan amesema kuwa ukatili mitandaoni umekithiri na inawaathiri viongozi wanawake kwa kiasi kubwa na madhara yake ni makubwa 

“Matusi,dharau na maneno yasiyo na staha ni mengi kwa wanawake kwenye mitandao ya kijamii hususan kwa wanawake waliopo kwenye siasa”

Amesema Rahima huku akisissita kuwa lengo la vuguvugu  wa ukombozi wa mwanamke ni “

Kukata mizizi inayomkwamisha mwanamke kufikia ndoto zake hivyo ni wakati  Taasisi zinazotetea wanawake kushikamana kutoa kauli moja ya kusisitiza mamlaka husika kulivalia njuga suala hili ili nawake wawe na amani na wapate haki yao.”Amemaliza Rahima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI