Header Ads Widget

MAKALA:WAJUMBE WANAWAKE KWENYE SHEHIA WALIVYOLETA MABADILIKO KAMATI ZA MAENDELEO PEMBA

Rais Dkt Mwinyi 

Na Fatma Hamad Faki Pemba.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. 

Uwepo wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000 na Mkakati wa Utekelezaji wake ya Mwaka 2005 unathibitisha dhamira ya wazi ya Serikali ya kukuza usawa wa kijinsia kama njia moja wapo ya kuimarisha ustawi na maendeleo ya watu wake.


Kamati ya Shehia wa Ngambwa iliyopo wilaya ya Chake Chake kuwa bado suala la usawa wa kijinsia halijazingatiwa ipasavyo,Wajumbe wa wanakamati hio ni 12, ambapo 8 kati ya hao ni wanaume na wanawake 4 tu.

Issa Rihan Abass ambae ni sheha wa Ngambwa amesema wanawake katika shehia yake hawajalipa kipaombele suala la uongozi na mkakati wake nikuhakikisha anatoa elimu ili kuondokana na hofu “Bado wanawake wa shehia yangu hawataki kujitokeza kushika uongozi kutokana na woga na dhana potofu za wanajamii juu ya wanawake na kuwa  viongoziAmesema Issa.

Hadia Omar Dadi ni Sheha wa Wingwi Njuguni,Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,kamati iliyopo katika shehia yake ina   jumla ya watu 10 ,ambapo sita na wanawake  ni wanne.Siku zote mwanamke anaweza kufanya vizuri popote atakapoekwa, kwani mama ni mwenye roho ya huruma na anayeweza kuleta maendeleoAmesema Hadia wakati akitoa maoni yake juu ya suala la wanawake kujitokeza kwenye kugombea nafasi za uongozi.

Wako viongozi wa wanaume wanaoamini kuwa mwanamke anauwezo mkubwa kwenye kuleta mabadiliko kama ambavyo Ali Omar Ali mwanakamati ya Shehia ya Wingwi Njuguni iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,amesema ushirikishwaji wa wanawake katika tasisi kunasaidia kupatikana kwa maendeleo  kwenye tasisi hizo.Mara nyingi anapopewa dhamana mwanamke pahala popote basi sio rahisi kufeli, kwani wanawake ni watendaji na ni waadilifu zaidi kuliko wanaume’’ Ali amefafanua.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kupitia kifungu chake cha 10 kifungu kidogo (e) kimeleza kila raia atakuwa na haki sawa, majukumu na fursa sawa kwa mujibu wa sheria.Ijapokua katiba yetu imeweka usawa kijinsia katika nyanja mbalimbali ikwemo katika vyombo vya maamuzi,utendaji, usawa huo haujazingatiwa ipasavyo.

Tukiangalia Zanzibar ina jumla ya Majimbo 50 ya Uchaguzi lakini kwa mujibu wa taarifa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 wawakilishi wanaume wanaongoza katika majimbo hayo jumla ni 42 wanawake ni nane (8) tu sawa na 16% tu ya wanawake katika majimbo yote ya Zanzibar.

Kwa upande wa mawaziri kwa mwaka 2024 ni 18 Wanaume wakiwa 12 wanawake 6 sawa na asilimia 33% ya Mawaziri wote huku Mawaziri wanaume wakiwa asilimia 77%.

Katika kuhakikisha suala la usawa kijinsia kwenye vyombo vya maamuzi linafikiwa ipasavyo wanaharakati na watetezi wa masuala hayo wamekuwa wakipiga kelele siku hadi siku kuona wanawake wanashirikishwa ipasavyo kwenye nyanja zote za uongozi, lakini bado usawa huo umekuwa ukisuasua.

Hali ya wanawake kuwa na idadi ndogo kwenye sehemu za maamuzi linaonekana pia kwenye Shehia ya Sizini,Iliyopo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskizini Pemba .Suleiman Shaame Hamad ni sheha wa Sizini amesema katika kamati yake amezingatia sawa wa kijinsia,wajummbe 10 waliopo hapo wanaume ni watano na wanawake ni watano.

Binafsi mimi mwenyewe nimeona nilipowashirikisha wanawake katika kamati yangu nimeona shehia yangu imepiga hatua kimaendeleo, na pia wananchi wameamka katika masuala ya kushiriki kwenye maendeleo Amemaliza Shaame.

Huko Shehia ya Bopwe iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskizini Pemba, nayo ni mfano mzuri wa kamati zenye usawa wa Kijinsia ambapo katika kamati hiyo wanawake ni watano na wanaume wanne.Sheha wa Shehia Bopwe Ramia Said Rashid amesema Kuwepo kwa usawa kijinsia kwenye kamati yangu kumepelekea kupatikana mabadiliko makubwa katika Shehia yangu tofauti na hapo awali ambapo idadi ya wanaume ilikuwa kubwa ikilingashwa na wanawake Amesema Ramia.

Sophia Ngalapi ni Afisa Mkuu wa Mahusiano kutoka Chama Cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA- Z), Chama ambacho kiko mstari wa mbele katika kuwapatia elimu na kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia kwenye vyombo vya maamuzi unakuwepo.


“Tukiangalia hata kwenye ngazi za shehia idadi ya Masheha wanawake ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya masheha wanaume ambapo masheha wanawake ni 81 tu kwenye shehia 388 sawa na asilimia 20 ya masheha wote Sophia ameendelea kusema kushauri kuwaTunatamani Sera isimamiwe na itekelezwe kwani siku zote wanawake ni wapenda amani, wapenda maendeleo, waadilifu, hivyo hata kwenye uongozi wao unakua ni hivyo hivyo wa mani, na utulivu Alimalizia Sophia.

Hafidh Abdi Saidi ni mwanaharakati kutoka Jumuiya ya Utetezi wa Kimazingira na Jinsia Pemb (PEGAO) amesema  baadhi ya Taasis tayari wamekuwa na uelewa wa kuwashirikisha wanawake katika uongozi na kuona juhudi zao kwenye hilo.

Tukiangalia hata kwenye kamati ya Tume ya Uchaguzi ya Bara ambayo imeundwa imezingatia usawa wa kijinsia,kwani ina jumla ya wajumbe 19, wanawake 12 na wanaume Saba tu Amesema Hafidh akitolea mfano wa Tume hio.

Mwanaisha Ali Masoud Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Pemba amesema bado Sera ya usawa wa kijinsia kwa baadhi ya tasisi haijatekelezwa ipasavyo na kutaka suala hili liwekewe mkazo kwenye utekelezaji. 

Tunataka kwamba kwa mfano wakiingia wanawake katika kugombea wasiwekwe chini wapewe nafasi sawa na wanaume kusiwe na upendeleo Amesema Mwanaisha.


   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI