Na Matukio Daima media
WAKATI Matokeo ya darasa la saba 2024 yakiwa yametangazwa mdau wa maendeleo Kilolo Aidan Mlawa amepongeza wazazi, walimu, na viongozi wa Mkoa wa Iringa wamepongezwa kwa usimamizi mzuri uliofanikisha ufaulu wa mtihani wa darasa la saba mwaka 2024.
Huku akisema pongezi nyingi kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira Bora ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kugharamia elimu bila malipo.
Hata hivyo anasema katika pongezi hizo uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa, Peter Serukamba, pamoja na wakuu wa wilaya zote umetajwa kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio haya.
Ufaulu huu umekuwa ishara ya heshima kwa mkoa na unatoa matumaini makubwa kwa mustakabali wa wanafunzi na elimu katika eneo hilo.
Wazazi wametakiwa kutumia fursa ya mafanikio haya kwa kuanza maandalizi mapema ya kuwaingiza watoto wao katika shule za sekondari mwakani.
Hamasa kwa wazazi ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto aliyefaulu mtihani huu anajiunga na kidato cha kwanza.
Aidha, wale ambao hawakubahatika kufaulu wanashauriwa kuandikishwa katika vyuo vya ufundi, kama vile RDO Kilolo na taasisi nyingine, ili wapate maarifa yatakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye.
Mdau wa maendeleo, Aidan Mlawa, amesisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan kupitia mpango wa kugharamia elimu bila malipo.
Mlawa amepongeza hatua ya serikali kuendelea kuboresha mazingira ya elimu nchini, jambo ambalo limeongeza fursa kwa watoto wengi kupata elimu bora.
Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya shule, kuwapatia walimu mafunzo ya mara kwa mara, na kuhakikisha vifaa vya kufundishia vinapatikana kwa wakati.
Kuwa mafanikio haya yameongeza matumaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wataweza kuendelea na masomo ya sekondari bila changamoto kubwa.
Viongozi wa wilaya nao wametakiwa kushirikiana na wazazi na walimu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto aliyefaulu anapata nafasi ya kujiunga na sekondari. Aidha,
Kuwa juhudi zinahitajika kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayekatizwa masomo kwa kukosa vifaa au mazingira stahiki ya kusoma.
Kuwa litaimarisha juhudi za mkoa wa Iringa kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa yenye kiwango bora cha ufaulu nchini.
Aidan Mlawa ametoa wito kwa jamii yote ya Iringa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha mafanikio haya yanaendelezwa.
Ufaulu wa mtihani wa darasa la saba mwaka huu unapaswa kuwa chachu ya maendeleo zaidi katika sekta ya elimu, si tu kwa mkoa wa Iringa bali pia kwa nchi nzima.
TAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA HAPA CHINI
👇
BOFYA LINK HII KUONA MATOKEO YOTE
0 Comments