Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewakaribisha wawekezaji na Watalii kutoka nchini Urusi kuwekeza nchini katika Sekta ya Maliasili na Utalii huku akisisitiza kuwa kupitia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Tanzania ni nchi salama na yenye amani.
Ameyasema hayo leo Oktoba 29,2024 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jijini Dar es Salaam.
“Huu ni wakati muafaka wa kujadili kuhusu masuala ya uwekezaji na maendeleo ya uchumi baina ya nchi hizi mbili na Tanzania tuna fursa nyingi za uwekezaji katika Hifadhi zetu na katika eneo la utoaji wa huduma za malazi na migahawa na bado tunahitaji watalii wengi zaudi kutoka nchini Urusi ikizingatiwa kwamba tawimu za mwaka 2023 watalii takribani 11, 655 kutoka Urusi wametembelea Tanzania” amesisitiza Mhe. Chana.
Kongamano hilo lililowakutanisha wawekezaji mbalimbali kutoka nchini Urusi pamoja na Wadau limefunguliwa na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Urusi, Bw. Maxim Reshetnikov na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo
0 Comments