Na Matukio Daima media
ZOEZI la uandikishaji wapiga kura limeonesha mafanikio makubwa, likidhihirisha imani ya Watanzania kwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuwa Serikali imeweka mazingira rafiki ya kidemokrasia yanayowahamasisha wananchi kushiriki katika michakato ya uchaguzi.
Akizungumza leo na Matukio Daima media mdau wa maendeleo Kilolo Aidan Mlawa alisema kuwa jambo hili linaloweka msingi thabiti wa kupata viongozi bora watakaoisaidia serikali kufanikisha malengo ya maendeleo na ustawi wa taifa.
Kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameendeleza sera za uwazi, maendeleo, na amani, zikilenga kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Alisema kuwa kupitia mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi na maboresho ya kiutawala, Watanzania wameonesha matumaini makubwa na ari ya kushiriki katika zoezi la uandikishaji, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada hizo.
Hivyo alisema uhamasishaji na umewezesha wengi wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanapata haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaofaa.
Mlawa alisema kupitia uandikishaji makini, Serikali inalenga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anashiriki kikamilifu katika kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo ya kweli.
Hivyo alisema kuwa viongozi watakaochaguliwa watakuwa na jukumu la kushirikiana na Rais Samia katika kufanikisha malengo ya taifa, hasa katika sekta muhimu kama afya, elimu, kilimo, na miundombinu.
"Ufanisi wa uchaguzi pia unategemewa kupanua fursa za wananchi kushiriki katika ujenzi wa uchumi shirikishi, unaotegemea maendeleo endelevu"
Hivyo alitaka wananchi kuepuka upotoshaji kutoka kwa baadhi ya wapinzani wasio na nia njema, ambao wanaweza kutatiza jitihada hizi kwa taarifa potofu na maneno yanayovuruga mshikamano wa kitaifa.
Alisema ni muhimu kwa kila Mtanzania kuelewa kuwa uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia unaowezesha kuchagua viongozi wanaotanguliza maslahi ya taifa.
" Serikali imehakikisha kuwa mazingira ya uchaguzi ni huru na haki, ili kila aliyejiandikisha awe na fursa ya kutumia haki yake ya msingi"
Alisema kila raia mwenye sifa, zoezi hili linaimarisha msingi wa demokrasia na ushirikiano wa pamoja kati ya viongozi na wananchi. Uandikishaji uliofanyika kwa mafanikio unatoa matumaini kuwa viongozi bora watapatikana, ambao watamsaidia Rais Samia kuendeleza juhudi za kuleta maendeleo nchini.
Hatimaye, Watanzania wanapaswa kuendelea kuwa na mshikamano na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa maslahi mapana ya taifa.
Kwa mujibu wa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema, takwimu zinaonesha kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 ambapo waliandikishwa wapiga kura 19,681,259 sawa na asilimia 86 ya lengo lililokuwa limewekwa la kuandikisha wapiga kura 22,916,412.
0 Comments