Header Ads Widget

TARI MARUKU WASHIRIKI VEMA KATIKA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Na Shemsa Mussa

 Kagera.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Maruku wameshiriki katika siku ya chakula Duniani huku wakiwapa elimu wananchi juu ya teknolojia bora ya uzalishaji na usindikaji wa chakula. 

Akizungumza katika viwanjwa vya CCM Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera yanapofanyika Maadhimisho hayo Dkt Mpoki Shimwela, Meneja kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania [Tari] Maruku amesema Maadhimisho hayo yanalenga Umuhimu wa Usalama wa chakula,upatikanaji wa chakula kwa watu wote duniani pia na kusisitiza kilimo endelevu.


Amesema kwa mantiki hiyo Malengo ya Maadhimisho hayo ni kazi zinazofanyika kila siku kwa taasisi hiyo, na wamekuja na aina nyingi za teknolojia za kilimo za mazao mbalimbali yanayozalishwa na taasisi hiyo ikiwemo zao kuu la Migomba. 

Pia amesema katika siku hiyo Tari Maruku wameweza kushirikiana kwa pamoja na vituo vingine ikiwemo Tari Tumbi,Kihinga,Naliendele kwa kutoa elimu kwa baadhi ya mazao ikiwemo Mihogo ,Viazi,Mahindi Chikichi Mawese],korosho,karanga na ufuta pamoja na bidhaa nyingine zinazotokana na mazao hayo.




Dkt Mpoki amesema wao kama Tari kwa njia hiyo wanalenga Usalama wa chakula kwa kumfundisha Mkulima kulima na kusindika na kuweka usalama wa chakula hapo baadae na kujua Zaidi umuhimu wa kilimo endelevu na kilimo chenye tija Zaidi na kuizingatia kauli mbiu kwa vitendo.

Aidha ameongeza kuwa Mkulima anapokuja katika banda lao  anapata elimu kuanzia shambani mpaka usindikaji hivyo mazao yote yaliyopo na mengine ambayo hayapo mkulima anafundishwa, kuhakikisha mkulima anapata elimu na mbegu bora ambazo zimezalishwa na tafiti pamoja na mbegu zenye ukinzani wa wadudu na magonjwa na zenye uzaaji mkubwa ili kumuongezea tija mkulima. 

“Mfano hapa kuna hii Mikungu ya ndizi ni aina ya ndizi inaitwa Tariban4 hii ni ndizi ni matoke kabisa ambayo tumezalisha kwa kutumia njia za kawaida za uzalishaji na inastahimili magonjwa ya mnyauko,wadudu kiuka] yaani bungua migomba na minyoo na katika kuhakikisha mkulima anapata usalama wa chakula tunafanya mambo mengi mfano ikiwemo,kushirikiana na mkulima wakati wa uzalishaji wa mbegu za mazao na tunahakikisha tunazalisha mbegu na chakula chenye radha zinazoendana na radha zinazozalishwa na wakulima wa kawaida,amesema Dkt Mpoki”  

Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya siku ya chakula duniani yameanza Oktoba 10-16,2024 na kitaifa yanafanyika ndani ya Mkoa Kagera huku kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu ikiwa ni { Haki ya chakula kwa wote kwa maisha bora ya sasa na yajayo}.


   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI