Header Ads Widget

TAMWA NA TCRA WAZINDUA SAMIA KALAMU AWARDS KWA WAANDISHI TANZANIA ..


Andrew Kisaka  meneja huduma za Utangazaji  mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) akijibu swali la waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati wa kutangaza tuzo za Samia Kalamu Awards,kulia ni  mkurugenzi wa Chama Cha waandishi wanawake Tanzania (TAMWA) Dkt Rose Reubeni na kushoto ni mwenyekiti wa TAMWA Joyce Shebe 

Na Matukio Daima media 

KATIKA Kuhakikisha waandishi wa habari na vyombo vya habari Nchini vinaendelea kufanya kazi zenye tija kwa jamii ,Chama Cha  wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wamezindua tuzo za  Samia Kalamu Awards chini ya kauli mbiu "Uzalendo ndio Ujanja". 


Mkurugenzi wa TAMWA Dkt. Rose Reuben akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam alisema kuwa tuzo hizo  zimeanzishwa kwa lengo la kuhamasisha na kukuza uandishi wa habari unaojikita katika maudhui ya ndani yanayohusu maendeleo, uwajibikaji, uzalendo, na kuboresha taswira ya Tanzania.

Dkt Reuben alisema kuwa tuzo hizo zitahusisha wanahabari wa Tanzania wanaochapisha, kutangaza, au kurusha maudhui yao kupitia magazeti, redio, televisheni, majukwaa ya mtandaoni, na vyombo vya habari vya serikali.

 "Zitatambua kazi zilizochapishwa kati ya tarehe 1 Januari na 26 Oktoba 2024 Changamoto na Fursa za Kukuza Uandishi wa Ndani"alisema 

Katika mazingira ya sasa ya utandawazi, vyombo vya habari nchini vimekuwa vikijikita zaidi kwenye burudani na kuhabarisha huku makala za kuelimisha zikiwa chache. 


Kuwa  maudhui mengi yanayotangazwa yana asili ya nje na hayatimizi ipasavyo mahitaji ya hadhira ya ndani.

 Alisema ili kukabiliana na changamoto hizi, TAMWA na TCRA waliendesha mafunzo kwa waandishi wa habari, watangazaji, wahariri, na watengenezaji maudhui wapatao 2,054 kote nchini kwa muda wa miezi mitatu mwaka huu.

Akieleza lengo la tuzo kuwa licha ya mafunzo hayo, imeonekana ni muhimu kuanzisha tuzo ili kuwatambua na kuwahamasisha wanahabari na vyombo vya habari vinavyojitahidi kuchapisha makala zilizofanyiwa utafiti wa kina na zenye tija kwa taifa. 

"Tuzo hizi zimepewa jina la Samia Kalamu Awards kwa heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan, rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania."

Hivyo alisema kuwa tuzo hizo zitatolewa tarehe 20 Novemba 2024 na kutaja makundi ya tuzo hizo kuwa  zimegawanyika katika makundi matatu.

Kuwa itakuwepo tuzo Maalumu za Kitaifa,tuzo kwa Vyombo vya Habari na tuzo za Kisekta.

Hata hivyo alisema vigezo vya Ushiriki ni pamoja na Makala zinapaswa kuzingatia masuala ya maendeleo yanayoathiri maisha ya wananchi na fursa kutoka kwenye miradi mbalimbali.

Alisema Makala lazima ziwe zimetangazwa au kuchapishwa kwa Kiswahili au Kiingereza kupitia vyombo vya habari ndani au nje ya Tanzania.

"Mwandishi lazima awe Mtanzania na makala iwe imefanyiwa utafiti wa kina, ikiambatana na angalau vyanzo vinne"

Aidha alisema kazi zote zinapaswa kuwa za kipekee na zisizowahi kushindanishwa katika tuzo nyingine.

Akielezea kuhusu mchakato wa upigaji Kura alisema kura  zitapigwa kwa kutumia SMS kupitia namba ya short code 15200 na pia kupitia tovuti rasmi ya tuzo https://samiaawards.tz. 

Alisema upigaji kura utahusisha wananchi kwa asilimia 60 na majaji kwa asilimia 40.

Alisema mbali ya tuzo mshindi wa Samia Kalamu Awards atapata pesa na kuwa tuzo hizo ni endelevu.


Andrew Kisaka ni meneja huduma za Utangazaji TCRA alisema kuwa tuzo hizo ni chachu kubwa kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari kufanya kazi kwa weledi zaidi .

Alisema toka TAMWA na TCRA wametoa Mafunzo zaidi ya waandishi wa habari 2000 wamepatiwa Mafunzo hayo  lengo likiwa wanahabari 1000 kufikiwa na Mafunzo hayo.


Samira Yusuph na Matias Canal ni miongoni mwa waandishi walipapiwa Mafunzo hayo walisema wanaoona fursa kubwa ya Mafunzo hayo katika kuongeza weledi na ubora wa kazi za waandishi na vyombo vya habari Nchini .

Samira alipongeza TAMWA na TCRA Kwa kutoa Mafunzo kwa waandishi wa habari Nchini na kuja na Samia Kalamu Awards kuwa ni tuzo zitakazoongeza Kasi kwa waandishi kufanya kazi zenye ubora 

Samia Kalamu Awards zinalenga kuimarisha weledi, maadili, na uzalendo miongoni mwa wanahabari, huku zikiwa kichocheo cha maendeleo nchini wanahabari wanahimizwa kutumia fursa hii kuwasilisha kazi zao kupitia mifumo rasmi iliyotajwa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI