Header Ads Widget

SONGWE KUANDIKISHA WAPIGA KURA 617,300 SERIKALI ZA MITAA -CHONGOLO.

 

   MKUU WA MKOA WA SONGWE DANIEL CHONGOLO


Na Moses Ng'wat,Songwe.


MKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amesema kuwa mkoa huo unategemea kuandikisha jumla ya  wapiga Kura 617,300 katika Daftari la mkazi na kwamba maandalizi ya kuelekea kwenye zoezi hilo yamekamilika.


Chongolo amebainisha hayo,  leo Oktoba 10, 2024 wakati  akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kuutarifu umma kuhusu zoezi hilo muhimu.


Amesema kuwa, zoezi hilo la kujiandikisha litaanza kesho Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu,  ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili za jioni.


Chongolo ameongeza kuwa, Mkoa wa Songwe utakuwa na jumla ya vituo vya uandikishaji wapiga Kura 1,723 katika Halmashauri zote tano za Mbozi, Tunduma Mji, Momba, Ileje na Songwe.


"Maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hili la uandikishaji  yanaendelea kukamilishwa na wananchi wote wenye sifa wanapaswa kujitokeza ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuingia kwenye mchakato wa  kuchagua viongozi" amesisitiza Chongolo.


Aidha, Chongolo amesema uandikishaji huo utafanyika katika Vitongoji kwa ajili ya uchaguzi wa 

Mwenyekiti wa Kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa 

Kitongoji.


Kwa upande wa Mitaa amesema uandikishaji utafanyika katika Mitaa kwa ajili ya 

uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI