Header Ads Widget

SERIS FOUNDATION YAWAFUNDA WAHANDISI VIJANA NAMNA BORA YA KUBUNI MIRADI NA KUJIAJIRI



TAASISI ya SERIS Foundation imeendesha mafunzo ya siku Nne ya Ujasiriamali na Ubunifu kwa Wahandisi Vijana ilikuwaongezea namna bora ya kubuni miradi na kujiajiri wenyewe ili kuwa na matokeo chanya katika jamii ikiwa ni pamoja na kujiinua kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa Jijini Dar Es Salaam na viongozi wa Taasisi hiyo ya SERIS Foundation wakati wa kufunga mafunzo hayo ya Ujasiriamali na ubunifu kwa wahandisi vijana 120 kutoka Mikoa mbalimbali nchini yaliyofanyika katika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Oktoba 23-26, 2024. 

Mwenyekiti wa SERIS Foundation, Mhandisi Josephat Shehemba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, amesema kuwa, lengo la kuanzisha mafunzo hayo ni kupunguza idadi ya Vijana Wahandisi wenye kutegemea kuajiriwa pekee.

"Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wengi ambao wanahitimu lakini hawana mawazo ya kuwapeleka sehemu kwa ajili yakuendeleza ujuzi wao,

Kwa hiyo mafunzo haya ya siku Nne yamefanyika katika kuwajengea na kupokea mawazo ya kijasiriamali kutoka kwao na kuona njia sahihi ya kuwakutanisha na wadau." Amesema Mhandisi Josephat Shehemba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SERIS Foundation,CPA Deborah Wami amesema mafunzo yamelenga kuwajengea uelewa na uwezo Wahandisi hao Vijana waliosajiliwa na bodi ya Uhandisi Tanzania (ERB) namna ya kuweza kujijiri na namna bora ya kufanya Ujasiriamali na Ubunifu.

Aidha, amebainisha kuwa, wataendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa Wahandisi Vijana pamoja na wadau wengine.

Kwa upande wake Msajili msaidizi wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali NGO's kutoka Wilaya ya Ilala Mwanaisha Ally amewasihi vijana hao kujiunga katika vikundi na kuomba mkopo unaotolewa na Halmashauri huku baadhi ya Wahandisi walioshiriki katika mafunzo hayo wakiahidi kutekeleza kwa vitendo kile walicho jifunza. 

Nae Mhandisi Davis Philipo mshiriki mafunzo hayo, ameishukuru SERIS Foundation kwa mafunzo kwani yanaenda kuhamsha hali ya kuendelea kujifunza zaidi vitu vipya, kwani Dunia inaelekea katika akili mnemba (akili bandia) ama inayofahamika kama Artificial Intelligence (AI).






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI