Header Ads Widget

MDAU WA ELIMU JOSEPH GORYO ATATUA TATIZO LA MAJI SHULE YA SEKONDARI ANTHONY MTAKA




MDAU wa Elimu na ambaye amekuwa mstari wa mbele katika Maendeleo ya kusaidia Jamii Nchini, Bw. Joseph Goryo ameweza kutatua tatizo la chombo cha kuhifadhia maji lililokuwa likiwakabili Shule ya Sekondari Anthony Mtaka ya Halmashauri ya Busega, Mkoani Simiyu.


Bw. Goryo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maafali ya Nne ya Kidato cha Nne ya shule hiyo, ametatua tatizo la uhaba wa chombo cha kuhifadhia maji kwa kununua tanki lenye ujazo wa lita 5,000 ili kuwaondolea adha wanafunzi wa shule hiyo ambao wamekuwa wakifuata maji mbali.


Bw. Goryo, mbali na tanki hilo pia yupo mbioni kuhakikisha anashirikiana na wadau ilikuweza kupata tanki kubwa zaidi lenye ujazo wa lita 10,000.


Aidha, Akitoa neno kwa Wanafunzi hao, Bw. Goryo amewataka kujilinda na Utandawazi wa kidijitali ili kujiepusha na tamaduni za kigeni zinazomomonyoa maadili na badala yake wazingatie tamaduni za Kitanzania zenye maadili mema kwani Dunia imeharibika.


"Kuna hatari ya Vijana wengi wakimaliza shule na wasipokuwa makini hujikuta wametumbukia kwenye lindi la Madawa ya kulevya na vitendo vya ushoga na usagaji.


Nitumie fursa hii kuwaomba Wazazi kuwalinda Watoto wetu kamwe msiwaruhusu kulala chumba kimoja na Wageni.


"Hata kama ni ndugu msikubali, maana wanaweza kujikuta hao Wageni wanawafanyia watoto vitendo viovu vikiwemo vya kuwalawiti. Amesema Bw. Goryo.


Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Japhet Sirikwa Joseph amemshukuru mgeni rasmi kwa msaada huo ambapo pia amemuomba kuweza kumfikishia kilio cha ujenzi wa uzio wa shule kwa wadau ili kukabiliana na wanyama wakali ambao hutokea katika pori la Akiba la Kijereshi na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Mwalimu amesema Wanyama hao kama Simba, Chui na Tembo huingia shuleni hapo mara kwa mara na kuharibu miundombinu ya shule ikiwemo mabomba ya maji na Miundombinu mingine.


Ambapo ameweza kuwa, kutokuwepo kwa uzio kumekuwa kukihatarisha maisha ya wanafunzi wakati wa usiku hali inayozua hofu kwa wanafunzi wanaokaa kwenye kambi ya kujisomea kwa mitihani kutofanya vyema wakati mwingine.


"Shule yetu inamuingiliano wa Wanyama mfano tembo ndiyo makazi yao mara kwa mara hufika kutafuta chakula, huangusha miti na wakati mwingine ni hatari kwa Wanafunzi na Wananchi kwa ujumla.


Tunampongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali katika sekta ya Elimu, hivyo tunaamini kupitia mgeni rasmi na Wadau na Serikali yetu jambo hili litaenda kupatiwa ufumbuzi" . Amesema Mwalimu Japhet.


Lakini pia ameomba ujenzi wa nyumba hata moja ya Walimu, kwani waliopo ukaa mbali na hutumia gharama kubwa kila siku kufika na kuondoka shuleni.


Sekondari ya Anthony Mtaka ina Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha Nne, ilianzishwa rasmi mwaka 2018 ikiwa na jumla Wanafunzi 381 na Walimu (5) na madarasa 13 tu, lakini hadi sasa imeweza kufikisha Wanafunzi 1154 na Walimu 25, ikiwa na Vyumba vya madarasa 40, Maabara za kisasa (2) na Bwalo moja.


Aidha, shule hiyo imeendelea kuongeza ufaulu wake kutoka Wanafunzi 6 wa daraja la kwanza (division one 2021) na kufikisha Wanafunzi 15 wa (Division one 2023).







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI