Header Ads Widget

SERIS FOUNDATION YAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA UBUNIFU KWA VIJANA WAHANDISI


NA. ANDREW CHALE, MATUKIO DAIMA APP, DAR.

TAASISI ya SERIS Foundation yenye malengo ya kuleta mabadiliko chanya kwa Jamii, inaendesha mafunzo maalum Oktoba 23-26, 2024 Jijini Dar es salaam kwa Vijana Wahandisi ambao wamehitimu na kusajiliwa na Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB).

Mafunzo hayo yameanza mapema jana Oktoba 23, 2024, yamefunguliwa na rasmi na Msajili msaidizi wa Jiji la Ilala Bi. Mwanaisha Boffu aliyewasilisha salamu za Serikali ambapo pia amewakaribisha vijana hao kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali.

Nae Bi. Rose Isack kutoka ERB ambaye amemwakilisha Msajili wa Bodi hiyo, amewaelezea namna wanavyokuwa na fursa mbalimbali kwa Wanachama wake.

"Bodi inakuwa na fursa mbalimbali kwa wale ambao wamesajiliwa.

Hata mafunzo haya ambayo yanatolewa na Seris Foundation ni matoke ya wao kusajiliwa na ERB hivyo fursa ni nyingi tuendelee kuhimiza vijana wengine kukiunga. 

Kwa upande wake, CPA. Deborah Wami ambe ni CEO wa Seris Foundation katika ufunguzo huo, amewataka Vijana hao kutumia mafunzo hayo kama fursa ya wao kuanzisha vikundi ambavyo vitawapeleka katika hatua nyingine ya kuanzisha miradi yao binafsi na kuacha na dhana ya kuajiriwa.

"Mafunzo haya yakawe chachu ya nyie kwenda kuanzisha vikundi ambavyo vitawapeleka katika hatua nyingine kwa kuanzisha miradi yenu binafsi na kuacha na dhana ya kuajiriwa"Amesema CPA Deborah Wami.

Mafunzo hayo yanafanyika katika Chuo cha Technolojia cha Dar es Salaam (DIT) na yanatarajiwa kuhitimishwa Jumamosi ya Oktoba 26 pamoja na utoaji wa vyeti.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI