Header Ads Widget

MLAWA -PONGEZI KWA WANACHAMA WA CCM KWA KUSHIRIKI KATIKA KURA ZA MAONI NI MWANZO MWEMA KUPATA VIONGOZI BORA SERIKALI ZA MITAA




Na Matukio Daima media 

WAKATI Oktoba 23 mwana huu wanachama wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wametimiza haki yao ya kushiriki kura za maoni kupata wagombea watakaopeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji na Vijijini ,mdau wa Maendeleo Kilolo mkoani Iringa Aidan Mlawa apongeza mchakato huo kuwa ni hatua kubwa ya ushindi wa CCM.

Chama imara chini ya Mwenyekiti makini na Imara Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Wana CCM na watanzania wanaimani kubwa kwa kazi nzuri anayoifanya ndio maana hamasa ya ushiriki Uchaguzi ni kubwa.

"Nawapongeza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa kura za maoni, hatua inayolenga kupatikana kwa viongozi makini watakaosimama imara kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa"

Anasema kuwa  ushiriki huo ni ishara thabiti kwamba demokrasia ndani ya chama chetu imeendelea kuimarika, na kwamba mnaelewa umuhimu wa kuchagua viongozi bora watakaotekeleza majukumu yao kwa uaminifu na weledi.

Mlawa anasema imani ya Watanzania kwa CCM bado ni kubwa, jambo linalothibitishwa na ushiriki wa wanachama katika hatua hii muhimu ya ndani ya chama. 

"Tunaamini kuwa, licha ya changamoto mbalimbali zinazojitokeza, viongozi bora na wenye maono ya maendeleo bado wapo ndani ya CCM".

Anasema kuwa uchaguzi wa viongozi wa mitaa ni nguzo muhimu ya utawala wa karibu na wananchi, na hivyo kuwa na viongozi makini kutasaidia kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo yanaendelea kuimarika.

"Sipsi wadau wa maendeleo tuna imani kubwa kuwa viongozi watakaochaguliwa kupitia kura hizi za maoni wataendana na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuonyesha juhudi na uthubutu katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi"

Hivyo anasema wananchi wanapaswa kuendelea kuiunga mkono kazi nzuri ya Rais kwa kuhakikisha wanachagua viongozi bora katika ngazi za mitaa. 

Kwani viongozi hawa si tu wawakilishi wa chama chetu, bali pia wanakuwa kiungo muhimu katika kuleta mabadiliko yanayoonekana moja kwa moja katika maisha ya kila siku ya Watanzania.

"Nawasisitiza wanachama na wananchi kwa ujumla kuendelea kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi kwa amani na utulivu"

 Kuhusu ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa viongozi wa mitaa  anasema si fursa tu ya kuchagua viongozi wanaowawakilisha, bali pia ni sehemu muhimu ya kudumisha demokrasia ya kweli. 

Mlawa anasema kuwa kura yako ina maana kubwa katika kujenga uongozi wenye dhamira ya kuwahudumia wananchi kwa haki, usawa, na uwajibikaji.


Aidha anasema ni wazi kwamba ushindi wa CCM katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa utaimarisha juhudi za Rais Samia na serikali kwa ujumla katika kusukuma mbele maendeleo.

 Hivyo ni  muhimu kwa wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wa CCM kwa lengo la kujenga taifa imara lenye ustawi na maendeleo ya kweli kwa kila Mtanzania.

"Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM"anasema Aidan Mlawa mdau wa Maendeleo Kilolo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI