Header Ads Widget

RC DENDEGO: SERIKALI YA AWAMU YA SITA INATUFURAHISHA WATENDAJI,INAFANYA KAZI KISAYANSI


Na Thobias Mwanakatwe, IKUNGI

MKUU wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego, ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kutokana na kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo hali ambayo inarahisisha kazi kuwa rahisi kwa watendaji serikalini.

"Serikali yetu ya awamu ya sita inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatufurahisha sisi watendaji inakwenda kisayansi zaidi yaani tunapotaka kufanya jambo yenyewe inatangulia hapa tunavyozungumza wilaya zote zimepata fedha kwa ajili ya kujenga shule mpya kabisa,fedha zipo kwa Wakurugenzi wote tayari wana fedha," amesema Dendego.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo leo (Oktoba 11, 2024) baada ya kutembelea ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Puma wilayani Ikungi akiongoza kamati maalum ya kukagua miradi akiwamo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata.

Dendego amesema serikali hii inatenda kazi hadi kupitiliza na kurahisisha kazi hivyo jukumu pekee kwa watendaji ni kuhakikisha miradi ambayo inapata fedha inasimiwa na kukamilika kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Martha Mlata, amempongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari Puma kwa kuonyesha uadilifu kutokana na kukamilisha majengo ya shule hiyo na kubakiza fedha.

Amesema wanafunzi wakazane kusoma kwani serikali imewajengea shule nzuri ambazo zinatoa nafasi nzuri kusoma ukilinganisha na miaka ya nyuma ambako wanafunzi walisoma katika shule ambazo hazikuwa katika mazingira mazuri.

Aidha,Mlata amesema wawekezaji kama  Barrick ambao wamechangia katika ujenzi wa Sekondari hiyo wanafanya hivyo kutokana na serikali ya awamu ya sita kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI