Header Ads Widget

RAIS SAMIA AWEKA MILIONI 585.2 KWENYE ELIMU MEATU


Na. MATUKIO DAIMA APP, MEATU.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwagusa wananchi baada ya kuweka kiasi cha Shilingi Milioni 585,280,028 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kisasa ya Sekondari Wilayani Meatu mkoani Simiyu.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika mapema Oktoba 27, 2024 na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kwa niaba ya Rais Samia ambapo pia aliwasilisha salamu kwa Wananchi hao wa Meatu.

Imebainishwa kuwa, Shule hiyo ya Kata ya Mwanuzi ina madarasa nane, ikiwemo jengo la Utawala, Maabara tatu, vyoo 10, chumba cha Kompyuta, Maktaba na sehemu maalum ya kuchomea takataka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI