Header Ads Widget

MUME ANAYEDAIWA KUUA MTALAKA WAKE NAE AFARIKI AKIPATIWA MATIBABU.

 


Na Moses Ng'wat, Songwe.

MUME anayedaiwa kusababisha kifo cha Mtalaka wake, Wema Ndile (32) baada ya kumshambulia kwa kumchoma visu, Ally Mwakilembe (45) naye amefariki dunia chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Oktoba 18,2024 imeeleza kuwa, mtuhumiwa huyo alifariki dunia Oktoba  17, 2024 majira ya saa  3:30 katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada naye kujijeruhi kwa kujichoma na kisu tumboni punde baada ya kuumua mtalaka wake.

"Ni kwamba mnamo Oktoba 15, 2024 majira ya 4:30 usiku, huko Kijiji cha Kapeta Ally Joseph Mwakilembe (45) alimshambulia kwa kumchoma Visu Wema Angolile Ndile (32) sehemu za shingoni na ubavuni upande wa kulia akiwa nyumbani kwake na kusababisha kifo chake".

"Baada ya tukio hilo, Ally Joseph Mwakilembe naye alijichoma kisu tumboni na kujisababishia jeraha ambapo alikimbizwa HospitalI ya Wilaya ya Ileje na ilipofika Oktoba 17, 2024 saa 09:30 alfajiri alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hosptalini hapo na wawili hawa walikuwa ni mke na mume" ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo ya polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni kwamba wawili hao  walitengana miezi mitano iliyopita ambapo mke aliamua kwenda kuishi sehemu nyingine kwa kujipangia chumba.

Awali taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa kijiji cha Kapeta, Octatus 

Wangu, ilidai kuwa kabla ya mauaji hayo kutokea, mtuhumiwa alikuwa katika harakati za kumshawishi mtalaka wake amrudie baada ya kutengana kwa miezi mitano.

Alisema kuwa, ndoa ya wawili hao ilidumu kwa kipindi cha miaka 10 na kufanikiwa kupata watoto wawili, lakini baadae mwanamke aliamua kutengana na mumewe akimtuhumu kuzidisha ulevi na kusahau majukumu ya familia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI