MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, NURDIN BABU
Na Esther Machangu, Moshi, Kilimanjaro
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Mkuu wa mkoa wa Kilimamjaro amewataka wakazi wa mkoa huo kushiriki katika zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Nurdin Babu ameyasema hayo leo October 10,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hao.
Babu amesema nchi yetu ya Tanzania ni nchi huru na kidemokrasia ambapo wananchi wanapaswa kuamua namna ya kuendesha maswala ya msingi katika serikali zao za mitaa
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amesema serikali ya awamu ya sita nchi ya uongozi wa Raisi Samia suluhu Hassan kupitia kwa waziri wa nchi, ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa(OR TAMISEMI) imeshatoa Tangazo na Ratiba ikishiria kianza kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Katika Tangazo hilo limebainisha Muda wa kujiandikisha kwa mpiga kura na mgombea ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 11 oktoba 2024 hadi tarehe 20 oktoba 2024 katika vituo vya kujiandikishia vipatavyo 2368 Mkoani hapa. Na muda wa kufungulia wa vituo hivyo ni saa mbili kamili asubuhi na kufungwa saa 12 kamili jioni na uwandikishaji huo utafanyika kwa muda wa siku 10.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa amesema baada ya uwandikishaji katika Daftari la orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi kutakuwa na zoezi la kukagua orodha ya wapiga kura ambapo orodha yote ya wapiga kura katika kitongoji au mtaa itabandikwa ili kutoa nafasi kwa wananchi waliojiandilisha kutoa pingamizi katika uandikishaji wa majina hayo.
0 Comments