MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew kwa kushirikiana na serikali wameboresha miundombinu ya elimu kwa kujenga nyumba ya walimu katika Shule ya msingi Ihula iliyoko kata ya Gibishi, wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, kwa gharama ya shilingi Mil. 92.3.
Imeelezwa kuwa lengo na ujenzi huo ni kuboresha makazi ya walimu, na kwamba katika ziara yake ya Agosti 1, 2024, Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, alishuhudia hali mbovu ya nyumba hizo, ambazo zilijengwa kwa udongo na hazikuwa na mazingira mazuri ya kazi.
Katika ziara hiyo, Mhandisi Kundo alizungumza na walimu na wanafunzi na kusisitiza juu ya umuhimu wa mazingira bora kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora ambapo aliahidi kuimarisha miundombinu ya shule hiyo kwa kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya walimu.
Katika kufanikisha hilo, Serikali imetoa kiasi cha shilingi mil. 92,300,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya za walimu (two in one - 2in1).
"Hadi sasa, zaidi ya walimu 8 wanapata malazi bora, hali ambayo inawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuchangia katika maendeleo ya wanafunzi." Amefafanua Mhandisi Kundo.
0 Comments