Header Ads Widget

HUDUMA YA WAHURUMIENI IMETOA MSAADA KWA WAZEE WENYE CHANGAMOTO YA KUPOTEZA VIUNGO WILAYANI ARUMERU.

 


Na,Jusline Marco,Arusha

Huduma ya Wahurumieni iliyo chini ya Mwambuli wa AGIVA  jijini Arusha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameweza kukabidhi msaada kwa wazee wenye ugonjwa wa Ukoma ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo katika kituo cha UPENDO LEPROSY HOME kilichopo eneo la Maji ya Chai Wilayani Arumeru, Mwasisi wa huduma hiyo Bi.Agnes Mayagila amesema AGIVA imekuwa na utaratibu wa kutembelea wahitaji ikiwemo watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu,wazee na wajane.

Miongoni mwa msaada waliokabidhi ni Mchele,mahindi,mafuta ya kupikoa,nguo na sabuni pamoja na fedha ambapo kwa kushirikiana na wanajamii wenye moyo wa huruma lengo likiwa ni kumshukuru Mungu kwa wale ambao wametoa baadhi ya vitu.

Amesema kubwa zaidi katika msaada huo ni sehemu ya kuifanya jamii kutambua kuwa wapo baadhi ya watu wenye uhitaji ili iwe sababu ya wao kutoa msaada ambapo ni matumaini yao kuwa wadau mbalimbali wataunga mkono juhudi hizo na kuunga mkono saerikali kwa kuwajali wahitaji.


"Sisi kama AGIVA kupitia huduma ya Wahurumieni  tunamshukuru Mungu kwa amekuwa msaada kwetu kukubalika kwenye jamii ili kwamba na sisi tuweze kuwashika mkono angalau kwa sehemu kubwa kidogo."Alisema mwasisi huyo

Kwa upande wake Siater Konstansia Mringi kutoka Shirika la Precious Blood wakati akipokea msaada huo amesema mpaka sasa kituo hicho kimeweza kuhudumia wazee zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali ambapo baadhi yao wametangulia mbele za haki huku wengine wakiwa bado kituoni hapo.

Amesema kituo cha UPENDO LEPROSY HOME kilianzishwa mwaka 1998 chini ya Bi.Feckren mwanachama wa Rotary Club ambapo mwaka 2003 kituo hicho kilikabidhiwa kwa wamissionary ili waweze kuhudumia zaidi wazee ukiachilia mbali changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo.

Ameongeza kuwa wito na utume wao ni kuhudumia wazee na makundi mengine yenye uhitaji kama watoto yatima ambapo ameishukuru huduma ya Wahurumieni chini ya mwamvuli wa AGIVA kwa kujitoa kwao na kusema kuwa msaada huo ni moja ya uinjilishaji kwa watu wenye uhitaji.

Sister Konstansia ameeleza kuwa uwepo wa kituo hicho umezingatia sheria zote za serikali ambapo wamekuwa wakishirikiana bega kwa bega na Halmashauri ya Meru kutambua idadi ya wazee walioko katika kituo hicho na maeneo walikotoka kusudi kuweza kuwasaidia ambapo amewaomba wadau wengine wenye mapenzi mema waweze kujitoa na kuwasaidia wazee hao ambao wengi wao wanahitaji matibabu,viatu maalimu na viti mwendo tiba.

Akizungumza kwa niaba ya wazee hao Eliminata Matei kutoka Geita wameishukuru huduma hiyo kwa msaada walioutoa kwao kwani umegusa mioyo yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI