Header Ads Widget

MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE , KUANZA KUTOLEWA MANISPAA YA BUKOBA .

 

TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Na Mariam Kagenda,Kagera

 ­­­­­Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Ndg. Jacob S. Nkwera leo tarehe 3/10/2024 ametangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na dirisha hilo likitarajiwa kudumu mpaka tarehe 3/11/2024.

Tangu kufunguliwa kwa mikopo hii ya Halmashauri, Bukoba Manispaa kwa mwaka  huu ina jumla ya TSH. 627,912,540.09 na vikundi vitakavyopewa mkopo ni lazima viwe vimesajiliwa na vimeomba mkopo kupitia mfumo wa WEZESHA PORTAL  kwa kutembelea tovuti  ya mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz

Aidha, vikundi hivyo vitakavyoomba mikopo vinatakiwa kuwa na sifa kama vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyosajiliwa na kupewa cheti na Halmashauri, vikundi hivyo kujishughulisha na shughuli za ujasiliamali  sambamba na kikundi cha wanawake na vijana kiwe na idadi ya watu kuanzia watano na kuendelea wakati huohuo kikundi cha watu wenye ulemavu kikiwa na watu wawili.

Kadhalika, kwa kuzingatia kanuni ya 6a (1) mtu mwenye ulemavu anaweza kuwa na sifa ya kupata mkopo kama kikundi cha watu wenye ulemavu iwapo timu ya menejimenti ya Halmashauri itajiridhisha kuwa amekosa mtu mwenye ulemavu wa kuungana nae katika eneo lake.

Masharti mengine ni uwepo wa akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina la kikundi, wanakikundi kukidhi takwa la uraia na kwa upande wa vikundi vya vijana, vijana hao kuwa na umri wa miaka kuanzia 18-45. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI