Header Ads Widget

MIAKA 60 YA HIFADHI YA TAIFA RUAHA

 

Uhifadhi, Utalii na Jamii.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Shigeki Komatsubara (ndani ya gari) akijaribu kuiendesha gari hiyo aina ya “Land Cruiser Pick Up” lililotolewa na shirika hilo kupitia Mradi wa SPANEST mwaka 2013 kwa ajili ya shughuli za ulinzi wa maliasili (doria) ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.


Mbali na msaada huo pia shirika hilo la kimataifa lilitoa mtambo mmoja (Grader) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara ambayo ilikuwa chachu ya kuongeza kasi ya ukuaji wa utalii, Mafunzo ya kutembeza wageni kwa miguu (walking safari’s), Mfumo wa Mawasiliano ya Radiocall kwa ajili ya doria na Mafunzo kwa vikosi maalumu vya doria ili kupunguza athari za ujangili ndani ya hifadhi hiyo.


Akimkaribisha katika Makao Makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo Msembe takribani kilometa 130 kutoka Iringa mjini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Meing’ataki alisema kuwa Komatsubara pia atashiriki zoezi la kutoa misaada kwa jamii inayopakana na hifadhi, huku shirika analoliwakirisha la UNDP watatoa mabegi 500 yanayotumia umeme wa jua kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la Nne na la Saba wanaojiandaa na mitihani yao.


Zoezi hilo la kutoa misaada hiyo litakalofanyika kesho tarehe 06.10.2024 katika kijiji cha Tungamalenga ni mwendelezo wa wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Ruaha ambapo hafla ya kilele hicho itafanyika tarehe 07.10.2024 huku mgeni rasmi akitajwa kuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI