Na Hadija Omary ,Lindi
Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe: Salma Rashid Kikwete ameshiriki zoezi la uandikishaji katika daftari la Mkazi, Kijiji cha Ruvu kitongoji cha Makasini kata ya Mchinga Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi
Akizungumza na viongozi wa chama pamoja na wananchi wa kijiji cha Ruvu Leo oktoba 17/2024 mara baada ya kushiriki Katika zoezi hilo la uandikishaji Mheshimiwa Salma kikwete ametoa Rai kwa wananchi kujitokeze kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la mkazi sambamba na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa seriali za mitaa, vijiji na vitongoji ifikapo tarehe 27/11/2024.
Hata hivyo Mama Salma alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake wa jimbo la Mchinga kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zilizotangazwa katika uchaguzi huu wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
0 Comments