MWENYEKITI wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard amepongeza jitihada kubwa za waandishi wa habari mkoa huo katika kuripoti vema maadhimidho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Akitoa pongezi hizo Leo wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru waandishi wa habari walishiriki kuripoti maadhimidho hayo .
Leonard alisema kuwa kazi iliyofanyika ni kubwa na nzuri ambayo imeheshimisha IPC pia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Hivyo alisema jitihada hizo ni kubwa na zinapaswa kuendelea kufanyika na waandishi wa habari mkoa wa Iringa hasa katika kuandika habari zenye tija kwa jamii.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Godwell Ole Meing'ataki alisema juhudi kubwa zimefanyika na vyombo vya habari mkoa wa Iringa.
Japo alisema si mara ya kwanza kwa vyombo vya habari mkoa wa Iringa kufanya kazi nzuri na kwa moyo pasipo kujali maslahi .
"Si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari mkoa wa Iringa kupongezwa kwani mara kadhaa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii zaidi"
Hivyo alitaka moyo huo wa kujituma kwa waandishi wa habari mkoa wa Iringa ni moyo wa kizalendo na kutaka moyo huo kuendelea ili kuendelea kuitangaza hifadhi ya Ruaha ili kuvutia zaidi watalii kutembelea Hifadhi hiyo .
Hata hivyo aliwataka waandishi wa habari kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kutangaza utalii nchini .
Kuwa Rais Dkt Samia amefanya kazi kubwa na nzuri ya kutangaza utalii nchini hivyo ni wajibu kuendelea kumuunga mkono kwa jitihada hizo.
Mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) amewataka wanahabari kuendelea kufanya kazi kwa kujitoa ili kukuza taaluma zao na kufikisha habari sahihi kwenye jamii.
Pia, amewapongeza waandishi Waliofanya kazi za maadhimisho ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa juhudi, bila ya matarajio ya kupokea malipo yoyote.
Amesema katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa walitoa jumla ya Makala na habari 174.
Hata hivyo, mwandishi wa habari toka Matukio Daima media, Francis Godwin ameibuka kuwa mshindi kwa kuandika Makala 40 na habari 14 za maadhimisho hayo.
Kwa upande wake, Francis Godwin, ameshukuru uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kuona mchango wa wanahabari katika kufanikisha maadhisho hayo, huku akiwa kumbusha waandishi kudumisha ushirikiano kati Yao ili kufikia malengo yao.
0 Comments