Header Ads Widget

MAJALIWA AAGIZA MJI WA MILOLA KUJENGWA BARABARA YA LAMI


  Na Hadija Omary 

Waziri Mkuu kasimu Majaliwa Majaliwa amemuaguza Meneja wa wakala wa Barabara Tanroads MKoa wa Lindi kuweka lami kipande Cha barabara  chenye urefu wa kilometa nne Katika kata ya Milola Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi 

Waziri Mkuu ametoa agiza hilo Leo oktoba 18,2024 wakati akisalimia wananchi na wakazi wa kijiji cha Milola A akielekea Jimboni kwake Wilayani Ruangwa.

Majaliwa Amesema ujenzi wa Barabara hiyo ya lami uende sambamba na uwekaji wa taaza barabarani ili ziweze kupendezesha mji huo.


"Na kwa kuwa alishaagiza kwa eneo lolote litakalojengwa barabara za lami , isiishie lami pekee lazima niwekwe na taa na Milola nataka ziwekwe hii itasaidia kupendezesha mji na hata kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi hawa "



Meneja wa tanroads Mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Silas amesema barabara hiyo mpaka kukamilika kwake  inakadiliwa kutumia Fedha zaidi ya shilingi Bilioni 3.5 ambazo tayari zimeshatolewa na setikali


 Mhandisi Silas amesema  kuanzia Jumatatu ijayo Oktoba21, 2024 wataalam wataenda kwenye kata hiyo ili waweze kuanza kazi ya usanifu na hatua nyingine za msingi zitaendelea ili baada ya mwezi mmoja, mkandarasi aanze kazi.




Awali mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi Mama Salma kikwete alimuomba Waziri majaliwa kuona uwezekano wa barabara za Jimbo hilo kuingizwa kwenye mtandando wa barabara za lami ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kusafirisha Bidhaa na wao wenyewe kwa urahisi


" Heshimiwa Waziri Mkuu Jimbo la Mchinga halina kipande cha lami Hata kipande cha sentimita moja kilio cha wananchinga kuwa na lami na hasa kwa barabara hii kutokea Ngongo mpaka Ruangwa hii ni changamoto kubwa ya wanamilola"

Hata hivyo Mama Salma kikwete alisema kuwa changamoto ya ujenzi wa barabara hiyo ni ilikuwa ombi kwa wananchi HAO walilolitoa kwa Waziri Mkuu kasimu majaliwa wakati wa kampeni 2020 lakini bado mpaka sasa changamoto hiyo haijapata ufumbuzi



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI