Madaktari bingwa na wabobezi 55 wa Mama Samia wamepokelewa mkoani Pwani tayari kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa katika halmashauri Tisa za mkoa huo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Madaktari hao bingwa na wabobezi Ofisini kwake Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani Dkt. Kusirye Ukio Boniface amesema Madaktari hao ni mabingwa katika kuhudumia Wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na afya ya kinywa na meno, presha ya kupanda, huduma ya ubobezi katika usingizi na usingizi salama, huduma ya mama na mtoto, upasuaji na mifupa, wakunga wabobezi, manesi wabobezi katika nyanja mbalimbali.
Dkt. Ukio alisema watakuwepo kwa siku tano yaani jumatatu mpaka ijumaa ambapo hii ni awamu ya pili kwa mkoa wa Pwani kupokea Madaktari hao bingwa na wabobezi ambao wanaenda kushiriana na watoa huduma wengine katika vituo vilivyopo katika mkoa wa Pwani.
Alisema "ieleweke kwamba tayari serikali imeshafanya mengi katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma, huletaji wa vifaa vya kisasa pamoja na kuongeza idadi ya watumishi katika maeneo ambayo serikali imefanya maboresho hayo.
Alisema kwasasa wanaenda kujikita katika hasa za kibingwa katika ngazi ya afya ya msingi"zoezi hili Lina lengo kubwa la kuboresha huduma kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa wale ambao wapo kwenye vituo husika ilikuongeza huduma katika maeneo hapo awali huduma hizo hazikupatikana.
Dkt. Ukio alisema Uongozi wa mkoa tayari umefanya maandalizi kwa kuhamasisha wananchi kujitokeza na wamewatayarisha watumishi sambamba na kuandaa Uongozi wa kuwapokea huko wilayani wataalamu hao.
Alisema pia wataalamu na Madaktari mabingwa wa ndani ya mkoa wanaendelea kufika katika vituo hivi ambavyo Madaktari mabingwa hao watakuwepo ili hata pale ambapo mazoezi haya hayaendelei ili kuwajengea uwezo na ufahsmu Kisha huduma za msingi nazo zinafikiwa na huduma hizo za kibingwa.
"Huko kwenye jamii kuna mahitaji makubwa sana ya huduma hizo za kibingwa hivyo tutajiwekea utaratibu wa kuwekeana zamu ili Madaktari wenu waende wakajifunze kwa kuhudumu pamoja nao ili wabadilishane uzoefu" alisema Dkt. Ukio.
Aidha amemshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya kukuwezesha madaktari wabobevu kwenda kutoa huduma kwa wananchi wa hali ya chini na ambao wamekua wakipitia changamoto ya kupata matibabu.
Mratibu wa Mradi huo kwa Mkoa wa Pwani Dkt. Michael Mbele amesema kuwa huduma hii ya Kampeni ya Mama Samia imelenga kuwafikia wananchi ambao hawana uwezo wa kuwafikia Madaktari Mabingwa Wabobevu wa maradhi ambapo watapata huduma zote za afya .
"Lengo kubwa ni kuwawezesha Wananchi wasiokuwa na uwezo wa kufikia huduma za kibingwa kwenye hospitali zetu kubwa wapate huduma hizo kwenye maeneo Yao"
Mganga Mkuu wa Halmshauri ya mji wa Kibaha Dkt Catherine Saguti amesema wamepokea magao wa Madaktari mabingwa wabobezi saba ambao watasaidia kitengo cha Wanawake na uzazi, Daktari bingwa wa watoto, ganzi salama na usingizi, bingwa wa upasuaji na mifupa.
Alimshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia kwa Halmshauri hiyo kupata billioni 4.5 kwaajili ya kuboresha huduma za afya na kujenga vituo vya afya na hospitali ya wilaya na kupata vifaa tiba vya kisasa.
DMO Bagamoyo Dkt. Kambi Lusingu amesema kuwa a amshkuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwatuma Madaktari Bingwa ambao wanakwenda kutoa huduma kwa wananchi na mafunzo kwa Madaktari wa Wilaya ya Bagamoyo ikiwa hii ni awamu ya pili kwa Madaktari wabobevu kwenda Bagamoyo tunatarajia kutatuliwa chagamoto za afya.
Alisema Madaktari mabingwa na wabobezi hao wanaenda kuondoa changamoto ambazo wananchi wa Halmshauri ya wilaya ya Bagamoyo wanapitia.
++++
0 Comments