Header Ads Widget

KUNENGE AHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

 


MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameongoza wananchi wa mkoa huo kwenye mbio za polepole (Jogging) kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi ujao.


Mbio hizo ambazo zilianzia kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa lilihusisha maelfu ya wananchi na kupita kupita baadhi ya maeneo ya mji wa Kibaha ziliishia kwenye ya zamani ya mabasi ya Maili Moja.


Kunenge amewataka wananchi kujiandikisha ili kupata fursa ya kuja kupiga kura ambapo zoezi hilo ambalo lilianza Oktoba 11 litaisha Oktoba 20 mwaka huu.


Amesema zoezi la kujiandikisha kwa wapiga kura ni muhimu kwani bila ya kujiandikisha mtu hataruhusiwa kupiga kura hivyo wajitokeze ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI