MNEC Salim Abri Asas
Na Matukio Daima media,Iringa
KAMPUNI ya ASAS Group yashinda tuzo kwa kuwa kampuni ya kwanza mkoani Iringa kwa ulipaji ankra za matumizi ya umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kampuni za Asas Group zinaongozwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC )Salim Abri Asas ambae ni mkurugezi zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya mkoa wa Iringa.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Iringa, Mhandisi Grace Ntungi, alieleza Leo kuwa zoezi la utoaji tuzo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambapo shirika lilikutana na wateja wake wakubwa wa umeme, jumla yao wakiwa 138, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili.
Hivyo mbali ya kupokea changamoto zao pia shiriki lilifanya tathimini kwa wateja wake na kuona ni vema kuwapongeza wale ambao wamekuwa walipaji ankra vizuri ambao wamekuwa Pato la Shirika.
Pamoja na kampuni ya Asas Group Kuongoza Kiwanda cha Karatasi Mufindi kimekuwa Cha pili na nafasi ya tatu ikienda kwa Kampuni ya Sao Hill.
" Tumekutana nao ili kuwaeleza mipango yetu, kusikiliza changamoto zao, na kuzitatua kwa haraka."
Aliongeza kuwa wateja waliopokea tuzo walichangia kwa kiasi kikubwa katika pato la shirika kwa ulipaji wa ankara kwa wakati na kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi makubwa ya umeme.
Meneja huyo alibainisha kuwa huduma ya umeme imeimarika sana kufuatia kukamilika kwa bwawa la Mwalimu Nyerere, ambalo limeongeza megawati 705 za umeme, hali inayosaidia kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wa mkoa huo.
Godfrey William, aliyepokea tuzo kwa niaba ya kampuni ya Asas, alilipongeza shirika kwa huduma bora na kutambua mchango wa kampuni yake.
Aidha, alisema kuwa Asas inaunga mkono juhudi za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi kwa ajili ya kulinda mazingira.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Venance Ntiadindura, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, alisisitiza umuhimu wa kudumisha mahusiano mazuri kati ya TANESCO na wateja wake kwa manufaa ya pande zote mbili, huku akiwakumbusha wateja hao kulipa ankara kwa wakati ili kusaidia shirika kutoa huduma bora zaidi.
0 Comments