NA WILLIUM PAUL, SAME.
ZIKIWA zimesalia siku tatu kuelekea kaunza zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi kuanzia Oktoba 11 hadi 20, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kumefanyika Jogging(mazoezi) maalum inayolenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki zoezi hilo.
Lengo ni kuhakikishw wanaweza kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27, mwaka huu.
Akizunguma wakati wa Jogging(mazoezi) hiyo iliyofanyika Kata ya Maore Jimbo la Same Mashariki, Mkuu wa Wilaya, Kasilda Mgeni amesisitiza Wananchi kuhakikisha ifikapo Octoba 11- 20 kila mmoja amhimize jirani, rafiki na familia yake kuzitumia vizuri siku hizo kumi ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa watakao wavusha kwenye miaka mitano ijayo.
“Uchaguzi huu ni muhimu sana ndugu zanguni na ndiyo maana leo tumeamua kufanya hii Jogging(mazoezi) ili kuwasisitizia umuhimu wa Uchaguzi wa mwaka huu, kwani unatoa dira ya Uchaguzi mkuu wa 2025 wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani”. Alisema Kasilda.
Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango amesema kuwa kwenye ziara zake alizofanya ndani ya Vijiji 46 kati ya 49 vilivyopo kwenye Jimbo hilo Wananchi wanafurahia sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wanangoja kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ijumaa ya Oktoba 11 – 20 ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa Novemba 27.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo Azza Karisha amesema kuwa sasa niwakati sahihi kwa kila mwananchi mwenye sifa kuchangamkia fursa ya uongozi kugombea nafasi mbalimbali kwenye Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Mwisho..
0 Comments